Wilaya
haukuwa mfumo uliofanywa na Allah Azza wa Jallah kwa ajili ya siku moja
au mbili, ulikuwa ni mfumo wa utawala kwa ajili ya Umma baada ya
kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w) mpaka siku ya hukumu. Mfumo huu pia
ulikuwepo kabla ya Ghadir na upo palepale daima. Vilevile madhumuni ya
kadhia ya Ashura yalikuwa ni kuurudisha Umma kwenye mhimili wa "Wilaya"
kwa vile watu walijitenga mbali na Ghadir. Wakati
watu wanajitenga mbali na Ghadir, Ashura inajitokeza. Vilevile moyo wa
Ashura ni "Wilaya." Wakati watu wanajitenga wenyewe mbali na "Wilaya"
walijitumbukiza kwenye Ukhalifa (Khilafat)", na kutoka kwenye "Ukhalifa"
mfumo ulibadilika kuwa Ufalme (Mulukiyat), na kutoka kwenye Ufalme
ulibadilika kuwa Uyazidi (Yazidiat). Viwango hivi vitatu vya uangukaji
chini vilitokea katika jamii baada ya kujitenga mbali na "Wilaya," na
Uyazidi (Yazidiat) ulikuwa msiba. Hapo ndipo Ashura ilipokuja na
kuwaambia watu kwamba ukombozi wenu upo tu kwenye "Wilaya." Mfumo wa
"Wilaya" upo mpaka siku ya hukumu. Hauwezi kusimamishwa kwa kifo cha
Mtukufu Mtume (s.a.w.w) wala kusimamishwa kwa ghaibu ya Maasum
(a.t.f.s). Ilikuwa ni uamuzi wa kimungu kwamba Mjumbe (s.a.w.w) lazima
afariki. Lazima aende kwenye ghaibu ya kudumu, lakini "Wilaya" ilikuwa
hai, ipo na mfumo huu ulikuwepo miongoni mwa Umma. Kama Maasum akienda
kwenye hali ya ghaibu kwa mda maalumu, bado mfumo wa "Wilaya" unaendelea
kuwepo, na hata kama Maasum akienda nyuma ya mapazia ya ghaibu kwa muda
usio na kikomo basi mfumo wa "Wilaya" bado unadumu. Hairuhusiwi sisi
kugeuza nyuso zetu mbali na Wilaya ima kwa sababu ya kifo cha Mtume
(s.a.w.w) wala kutokana na ghaibu ya Maasum. Na Ustadh Sayyid Jawwad
Naqvi