Ni kwa mda
gani ulimwengu utaziba masikio yake ili usisikilize umwagaji damu wa
Wapalestina mikononi mwa wavamizi? Je! Wapalestina hawapaswi kufurahia haki yao
ya kuishi kwa uhuru katika ardhi yao kama watu wengine ulimwenguni? Uhalisi wa
kimataifa ambao kwamba tulilinganiwa na ulimwengu kuutambua na kushikana nao
unakanyagwa kila siku katika Palestina na jeshi la wavamizi na ongezeko lake la
kijeshi na mazingira yanayowekwa katika miji yao, vijiji, kambi, na kusababisha
umwagaji wa damu wa Wapalestina kwa mashine pofu za kijeshi zilizokusudiwa kwa
ajili ya kuwaangamiza Waislamu na wasio Waislamu katika ardhi ya Palestina
pamoja na Masjid Al- Aqsa.