WAMOROCCO WAANDAMANA KUIPINGA ISRAEL.


Wananchi wa Morocco wamefanya maandamano kuiunga mkono Qudsi Tukufu na msikiti wa al-Aqsa na kuulani utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Maandamano hayo yaliyofanyika mjini Rabat uku yaliwashirikisha pia makumi ya wanasiasa wanaopinga utawala huo wa Kizayuni. Wakiwa mbele ya bunge la Morocco waandamanaji walilaani vikali mashambulizi ya askari wa Kizayuni dhidi ya Waislamu katika msikiti wa al-Aqsa na kuutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya utawala huo pandikizi. Maandamano hayo yameitishwa na jumbe tatu nchini Morocco zinazopinga kuendelezwa uhusiano wa nchi hiyo na utawala haramu wa Kizayuni. Aidha wandamanaji walitoa nara za kulaani njama za utawala huo za kutaka kuuyahudisha mji wa Qudsi Tukufu. Maandamano kama hayo dhidi ya utawala wa Kizayuni yalishuhudiwa pia mjini Tunis, Tunisia ambapo waandamanaji walichoma moto bendera ya utawala huo.