MKAPA AIKOSOA MISAADA YA WAMAGHARIBI AFRIKA.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amesema kuwa, misaada inayotolewa na madola ya Magharibi kwa nchi za Afrika haina masilahi na kwamba, lengo la kudhoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika .Mkapa amesema kuwa, kuwa mara nyingi nchi za Magharibi zimekuwa zikitoa misaada kwa masharti ya kutolewa kwa ushuru kwa bidhaa zinazoingia pamoja na bidhaa zinazouzwa katika mataifa hayo, jambo ambalo linaweza kudhoofisha ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesisitiza kwamba, masharti hayo yanapaswa kuepukwa na viongozi wa nchi za Afrika na kusisitiza kwamba hayo yanaweza kuepukika ikiwa mataifa hayo yatawekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha wanawaandaa vijana kwa kuwapatia elimu bora. Benjamin Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. (irib)