ANAYEPENDA KUISHI MAISHA ALIYOISHI MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W).

Imam Ali bin Abi Talib (a.s) amesema:

" Mnakwenda wapi na ni vipi mnadanganywa hali ya kuwa muongozo upo na Aya ziko wazi na minara imesimikwa, basi vipi mnapotoshwa bali ni jinsi gani mnapotea hali yakuwa miongoni mwenu kimo kizazi cha Nabii wenu ambao ni walinzi wa haki, na ndiyo muongozo wa dini na ndimi za ukweli, basi waheshimuni kwa heshima nzuri ya Qur'an na muwafuate kama ngamia mwenye kiu kali afuatavyo (maji). Enyi watu kichukueni kutoka kwa Mtume wa mwisho (s.a.w), hakika hufariki mwenye kufariki miongoni mwetu (sisi wa nyumba ya Mtume) lakini anakuwa hajafariki, na kuchakaa mwenye kuchakaa miongoni mwetu lakini siyo kwamba amechaka, basi msiseme msiyoyajua, kwani haki imo ndani ya vile mnavyovikanusha. Na toshekeni kwa mtu ambaye ninyi hamna hoja yoyote dhidi yake, nami ndiye huyo mtu, basi je, sikukitumia ndani yenu kizito kikubwa na ninakuachieni kizito kidogo nami nimesimika kwenu bendera ya Imani."
Rejea: Nahjul-Balaghah ya Imam Ali Juz. 1 Uk. 155