KUJIAMINI KWA IMAM ALI BIN ABI TALIB (A.S).


 Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alikuwa akifanya kitu akiwa na matumaini na uzuri wa matendo yake, huku akidhihirisha haki wazi wazi, kiasi kwamba hata Shujaa wa bara la Uarabu Amru bin Abdul Wuddi hakumzua kudhihirisha haki huku Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na Maswahaba wakimtahadharisha dhidi ya Amru. Hivyo ni dalaili inayoonyesha kujiamini kwake na Ushujaa wake mbele ya haki, vitu ambavyo vilijaa ndani ya nafsi yake.

Mara nyingi amekuwa akitoka kuelekea kwenye Swala bila ya kusindikizwa na mtu atakayezuia hatari za maadui mpaka Ibnu Muljimu alipomkuta na kumpiga na Upanga wenye sumu. Je, huu si Ushahidi juu ya kujiamini kwake mbele ya haki, kujiamini ambako kunaendesha viungo vyake vyote na mwenendo wake wote.

Kutokana na kujiamini huku kuzuri ndio maana anamwambia Swahaba wake na Gavana wake huko Madina Sahlu bin Hunayfa Al-Answariy kuwa: "Ama baada, zimenifikia habari kuwa watu kati ya wale waliokuwa kabla yao wanakwenda kwa Muawiyyah kwa siri, hivyo usihuzunike kwa idadi yao itakavyokupita wala kwa mchango wao utakaokutoka, kwani naapa kwa Mwenyezi Mungu wao hawajakimbia toka kwenye ujeuri wala hawajajiunga na uadilifu."

Rejea: Nahjul-Balagha, barua ya 70.