UKOMBOZI WA FALASTIN.

Katika vita vya Khaybara, 
tarekh inaonyesha kuwa: Mtume (s.a.w.w),alimpeleka kila kila mmoja katika 
Maswahaba, akampa bendera kwenda kupigana na Mayahudi, 
 hakuna aliyeshinda. Mpaka Mtume (s.a.w.w), alipompa bendera mtu ambaye ni Mpenzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Akaenda akapigana akashinda, Khaybar ikawa mikononi mwa Waislamu. Sasa, Mayahudi wamekita nguvu zao katika ardhi ya Falastin, tunawasikia kina Marhab wanajisifu na kujivuna na wanamdharau kila mtu. Wanaendesha mauwaji ya halaiki, na kuangamiza kila kitu.

Kwa hiyo, hili kuisafisha ardhi ya Falastin inahitajika mtu pekee atakaebeba bendera ya Ahlul-Bayt (a.s), aongoze jeshi kuikomboa Falastin.