MAHADHIMISHO YA QUDS YAFANYIKA KITAIFA MASJID MTORO, JIJINI DAR ES SALAAM, BAADA YA SALA YA IJUMAA.


HARAKATI ZA WAPALESTINA.

Hususani harakati zao za silaha- na uvamizi wa Al-Quds umeteka mawazo ya Waislamu. Ni kwa muda gani ulimwengu utaziba masikio yake ili usisilize umwagaji damu wa Wapalestina mikono mwa wavamizi? Je! Wapalestina hawapaswi kufurahia haki yao ya kuishi kwa uhuru katika ardhi yao kama watu wengine ulimwenguni? Uhalisi wa kimataifa ambao kwamba kwamba tulilinganiwa na ulimwengu kuutambua na kushikana nao unakanyagwa kila siku katika Palestina na Jeshi la wavamizi na ongezeko lake la kijeshi na mazingira yanayowekwa katika miji yao, vijijini, kambi, na kusababisha umwagaji wa damu wa Wapalestina kwa mashine pouf za kijeshi zilizokusudiwa kwa ajili ya kuwaangamiza Waislamu na Masjid Al-Aqsa
.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa Masjid Mtoro, Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuwakumbuka Waislamu wa Falastin kutokana naunyama wanaofanyiwa na Mayahud dhidi ya ardhi yao, Mwenyezi Mungu asiwahulumie watu hawa.

  
Katibu Mkuu wa Harakati 
za Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah Lebanon ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuuasa kwamba, usithubutu kuishambulia kijeshi Iran; kwani jibu la Tehran litakuwa kali mno. Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo katika hotuba yake kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds iliyoadhimishwa jana kote ulimwenguni na kuitaka Israel isianzishe chokochoko yoyote ile ya kijeshi dhidi ya Iran. Aidha Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amebainisha kwamba, licha ya njama zote za maadui, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesimama kidete na inazidi kupata nguvu siku baada ya siku. Nasrullah amezungumzia umuhimu wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kwamba, suala la Quds ni jukumu la kidini kwa Waislamu wote hivyo kuna haja kwa Waislamu kusimama kidete na kutetea kibla chao cha kwanza ambacho kinakabiliwa na njama za kila leo za 
Wazayuni maghasibu.