Leo tarehe 3-03-2016 maelfu ya watu wamejitokeza barabarani Bauchi,
Nigeria kwa ajili ya kuitaka serikali imuachie huru Sheikh Ibrahim
ZakZaky Kiongozi wa harakati ya Kiislam nchini humo.
Itakumbukwa
kuwa, tarehe 12 hadi 14 Disemba mwaka uliopita wa 2015, jeshi la
Nigeria lilishambulia kituo cha kidini na nyumba ya kiongozi wa Harakati
ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria na
kuua mamia ya Waislamu wasio na hatia. Hatima ya Sheikh Zakzaky ambaye
alipigwa risasi kadhaa katika hujuma hiyo, bado haijajulikana mpaka
sasa.