TUKIO LA GHADIR KHUM.


Waumini wa dini ya Kiislamu Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah jijini Tanga sehemu ya Pongwe, wameungana katika kukumbuka ya tukio la Kihistoria la Ghadir Khum, ambapo Mtume (s.a.w.w) aliuthibitishia ulimwengu wa walimwengu kuwa baada yangu Kiongozi na Khalifa kwenu atakuwa ni Ali bin Abi Talib (a.s). Alifikisha ujumbe katika hali ya kuunyanyua juu mkono wa Amirul Muuminina Ali bin Abi Talib (a.s) ambapo waislam wote waliohudhuria waliona kwa macho yao na kusikia kwa masikio yao Khalifa baada ya Mtume (s.a.w.w) ni Ali mwana wa Abi Talib (a.s). Sheikh Taqee Zachalia amewapongeza waliyoandaa kumbukumbu hiyo adhimu ili kulihuisha tukio hilo adhimu ambalo liliambatana na kukamilishwa kwa Dini yetu Tukufu ya Uislam,kutimizwa kwa Neema ya Mola wetu,pamoja na kupendelewa dini yetu iwe ni Dini ya Uislam.