VIKOSI VYA MAJESHI YA SHIA VYAANZA MASHAMBULIZI YA UKOMBOZI WA MJI WA ANBAR - IRAQ.


Baada ya jeshi la Marekani na washirika wake kuonekana kushindwa kupambana na kundi la kigaidi la Daesh, hatimaye jeshi la shia laanza rasmi mapigano ya ukombozi wa mji wa Anbara ambao umetekwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh.

Serikali ya Iraq imetangaza kuzinduliwa kwa operesheni ya kuukomboa mkoa wa Anbar ambako wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh waliteka mji mkuu mwezi huu, katika pigo kubwa kwa juhudi za Marekani kulitokomeza kundi hilo la kigaidi la Kisunni.

kundi la kigaidi la Daesh limeripotiwa kupeleka wapiganaji zaidi katika mji wa Ramadi, kujiandaa na mapambano hayo, huku Marekani ikihangaika kuihakikishia ushirikiano serikali mjini Baghad, baada ya afisa wa Marekani kuvikosoa vikali vikosi vya Iraq.

Wapiganaji kundi la kigaidi la Daesh walijiimarisha mjini Ramadi siku ya Jumatatu, kwa kupeleka wapiganaji zaidi kujiandaa na vita dhidi ya majeshi ya usalama na makundi ya wanamgambo yanayosonga mbele kuelekea mji mkuu huo wa jimbo la Anbar, uliopo umbali wa kilomita 110 kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.

Vikosi vya majeshi ya Shia vimerejesha baadhi ya maeneo mashariki mwa Ramadi tangu kuanzisha mashambulizi siku ya Jumamosi, wiki moja baada ya jeshi la serikali kufurushwa na kundi hilo la kigaidi la Daesh, na jana Jumatatu vikosi hivyo vya kishia vyenye kusifika kwa nguvu, uwezo na ustadi wa kupambana, vinavyodhaminiwa na na kufundishwa na majeshi ya Iran vilichukuwa eneo la vijiji kusini mwa mji huo kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi la Daesh.

Operesheni kuhusisha makundi mbalimbali

Kamanda wa operesheni za Mto Euphrates Meja Jenerali Qais Al Muhammadawi, amesema mashambulizi ya kuikomboa Ramadi yatahusisha jeshi la Iraq, wanajeshi wa Kishia na wapiganaji wa Kisunni.

Muhammadawi  alisema: "Ni eneo muhimu sana. Tuna idadi nzuri tu ya watu wanaolifahamu, marafiki wanalijua, makabila, jeshi, polisi, PMF, wote na sisi wote kundi hili linalopambana dhidi ya adui Daesh,".

Wakazi wa Ramadi waliripoti kuwa magari yaliyobeba wapiganaji wa Muhammadawi yaliwasili mjini humo siku ya Jumapili, na kuanza kuwatawanya kwenye maeneo mbalimbali. Abu Saed alisema aliwaona wapiganaji wa Muhammadawi wakishuka kwenye magari mawili na kukimbilia kwenye majengo na kujificha. Mkazi mwingine alisema aliona wapiganaji wasiopungua 40 wakiruka kwenye magari yaliyowasili katika wilaya ya kusini ya al-Tamim Jumapili jioni.

Katika matamshi aliyoyatoa kwa televisheni ya CNN siku ya Jumapili, waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter, alivikosoa vikosi vya Iraq kwa kushindwa kuidhibiti Ramadi, licha ya kuwa na idadi kubwa kuliko wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Matamshi hayo yalijibiwa kwa hasira na waziri mkuu wa Iraq, Heider Al.Abadi, ambaye aliliambia shirika la utangazaji la Uingereza BBC, kuwa waziri huyo wa ulinzi wa Marekani alipewa taarifa zisizo sahihi. Abadi alitabiri kuwa Ramadi itarejeshwa mikononi mwa serikali katika "muda wa siku tu."

Kukamatwa kwa mji huo na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh kutokana na uzembe wa majeshi ya Marekani ambayo yamekwenda Iraq kwa madai ya kuisaidia serikali hiyo kupambana na magaidi hao, lakini pindi magaidi hao walipokaribia mji wa Ramadi wanajeshi wa Marekani walihama kambi zao zilizopo katika mji huo na kusogea nyuma.

Marekani yahaha kurekebisha hali

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden alizungumza na Abadi jana, na taarifa ya ikulu ya White House ilisema Biden alitambua kujitolea kwa kiwango kikubwa na ushujaa wa vikosi vya Iraq katika kipindi cha miezi kumi na nane iliyopita mjini Ramadi na kwingineko, na kuongeza kuwa Marekani itafanya kila iwezelo kuvisaidia vikosi vya Iraq, yakiwemo makabila ya mkoa wa Anbar, ili kuwaondoa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh mkoani humo.

Kutekwa kwa mji wa Ramadi na mji wa kale ya Palmyra nchini Syria, ndiyo mafanikio makubwa zaidi ya kundi la kigaidi la Daesh tangu muungano unaoongozwa na Marekani ulipoanzisha mashambulizi ya angani dhidi yao mwaka uliopita. Ushindi wa karibu wakati mmoja dhidi ya majeshi ya Iraq na Syria umeilaazimu Marekani kutafakari upya mkakati wake wa mashambulizi ya angani, huku ikiacha mapigano ya ardhini kwa vikosi vya Iraq.

Majeshi ya Marekani ya ardhini yameshindwa kuonyesha mafanikio yeyote katika uwanja wa vita wa kupambana na magaidi wa Daesh, tofauti na vikosi vinayoongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran ambavyo vimeweza kuwashinda magaidi hao na kuwaondoa kwenye maeneo mengi ya Iraq. Chanzo cha habari: http://sw.abna24.com/service/important/archive/2015/05/26/692132/story.html