Hawakuweza kuelewa ile dhati ya “Wilaya” na wakati walipotakiwa kueleza maana yake, walitoa maelezo mepesi sana kama vile “Urafiki” au “Mapenzi.” Je, Mtume (s.a.w.w) baada ya maandalizi yote hayo na ushukaji wa Aya hizo, alikuwa anatangaza urafiki au mapenzi?
Huu ndio
wasiwasi uliomshughulisha Mtume
(s.a.w.w) kwamba Ummah unaweza ukaishiliza maana ya “Wilaya” mpaka kwenye
urafiki na mapenzi tu, hawatasonga mbele katika kuusimamisha kama mfumo.
“Wilaya” ni
mfumo wa Kimungu kwa ajili ya mwongozo wa Wanadamu. Ni mfumo bora sana ambao
una khususia (kazi maalum). Sina nafasi ya kuzitaja taaluma za mfumo huu hapa
na kuulinganisha na mifumo mingine ya utawala. Hili lilikuwa ni tangazo la
mfumo wa utawala wa Kimungu, lakini Ummah hawakuukubali katika njia hii,
waliutafsiri kimakosa. Hawa kwenda katika njia ile ambayo Mjumbe wa Mwenyezi
Mungu (s.a.w.w) alitaka waichukue. Hatua ya kwanza waliyochukua ilikuwa ni
kujitenga na “Walii” huyo. Wacha ajitokeze yeyote kutokana na “Answar”
(Wasaidizi wa Madina) au “Muhajirin” (Wahamiaji kutoka Makka) kuwa kiongozi,
lakini Walii wa kweli asijitokeze.
Wilaya
haukuwa mfumo uliofanywa na Allah Azza wa Jallah kwa ajili ya siku moja au
mbili, ulikuwa ni mfumo wa utawala kwa ajili ya Ummah baada ya kufariki Mtukufu
Mtume (s.a.w.w) mpaka siku ya hukumu. Mfumo huu pia ulikuwepo kabla ya Ghadiir
na upo palepale daima. Vile vile madhumuni ya kadhia ya Ashura yalikuwa ni
kuurudisha Ummah kwenye mhimili wa “Wilaya” kwa vile watu walijitenga mbali na
Ghadir. Wakati watu wanajitenga mbali na Ghadir, Ashura inajitokeza. Vile vile
moyo wa Ashura ni “Wilaya.” Wakati watu wanapojitenga wenyewe mbali na “Wilaya”
walijitumbukiza kwenye Ukhalifa (Khilafat)”, na kutoka kwenye “Ukhalifa” mfumo
ulibadilika kuwa Ufalme (Mulukiyat), na kutoka kwenye Ufalme ulibadilika kuwa
Uyazidi (Yazidiat). Viwango hivi vitatu vya uangukaji chini vilitokea katika
jamii baada ya kujitenga mbali na “Wilaya,” na Uyazidi (Yazidiat) ulikuwa
msiba. Hapa ndipo Ashura ilipokuja na kuwaambia watu kwamba ukombozi wenu upo
tu kwenye “Wilaya.”
Mfumo wa
“Wilaya” upo mpaka siku ya Hukumu. Hauwezi kusimamiswa kwa kifo cha Mtukufu
Mtume (s.a.w.w) wala kusimamishwa kwa ghaibu ya Maasum (a.t.f.s). Ilikuwa ni
uamuzi wa Kimungu kwamba Mjumbe (s.a.w.w) lazima afariki. Lazima aende kwenye
ghaibu ya kudumu, lakini “Wilaya” ilikuwa hai, ipo na mfumo huu ulikuwepo
miongoni mwa Ummah.
Kama Maasum
akienda kwenye hali ya ghaibu kwa muda maalumu, bado mfumo wa “Wilaya”
unaendelea kuwepo, na hata kama Maasum akienda nyuma ya mapazia ya ghaibu kwa
muda usio na kikomo basi pia mfumo wa “Wilaya” bado unadumu. Hairuhusiwi sisi
kugeuza nyuso zetu mbali na Wilaya Imma kwa sababu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)
wala kutokana na ghaibu ya Maasum.
Na Sayyid Jawwad Naqvi
Na Sayyid Jawwad Naqvi