Serikali halali ya Palestina iliyochaguliwa na wananchi na inayoongozwa
na Waziri Mkuu Ismail Haniya imetoa wito wa himaya ya kila upande kwa
msikiti mtakatifu wa al-Aqswa. Taher al-Nunu, Msemaji
wa serikali ya Palestina amewataka Wapalestina wote wajitokeze na
kuuhami msikiti mtakatifu wa al-Aqswa ambao unakabiliwa na hujuma za
kila upande za utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha Taher al-Nunu
ameutaka umma wote wa Kiarabu na Kiislamu kutekeleza majukumu yao
ipasavyo katika kuunga mkono na kuuhami msikiti huo mtakatifu wa
al-Aqswa. Msemaji wa serikali halali ya Palestina amesisitiza kwamba,
kuna haja ya kuweko himaya ya kila upande na Waislamu wote kwa Masjdul
Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Katika siku za hivi karibuni
utawala wa Kizayuni umezidisha vitendo vya kuuvunjia heshima msikiti wa
Al Aqswa jambo ambalo limewakasirisha Waislamu na wapenda uhuru kote
duniani. Utawala huo ghasibu aidha kila Ijumaa huwazuia vijana wa
Kipalestina kutekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika msikiti huo.
Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/31937-serikali-ya-palestina-yataka-himaya-kwa-msikiti-wa-al-aqswa