WANAHARAKATI UINGEREZA WAANDAMANA DHIDI YA RAIS WA NIGERIA, WATAKA KUACHIWA SH. ZAKZAKY.


Makundi ya waharakati wa kutetea haki za binadamu yamefanya maandamano katika mji mkuu wa Uingereza London kulalamikia dhuluma na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya usalama vya Nigeria dhidi Waislamu wa nchi hiyo.

Mwandishi wa kanali ya televisheni ya Press TV ya Iran ameripoti kuwa wanaharakati hao wametumia safari ya Rais Muhammadu Buhari nchini Uingereza kuandamana na kulaani ukandamizaji unaofanywa na serikali ya rais huyo dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika. Rais wa Nigeria yuko Uingereza kushiriki mkutano wa kupambana na ufisadi. Kadhalika wanaharakti hao wameitaka serikali ya Rais Muhammadu Buhari kumuachia huru msomi wa Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim Zakzaky. Wanaharakati hao wa kutetea haki za binadamu wanasema wimbi hilo la malalamiko ni utangulizi wa kuilazimisha serikali ya 

Abuja imwachie huru Sheikh Zakzaky.
Kumekuwepo wasiwasi mkubwa kuhusu ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Nigeria dhidi ya Waislamu hususan wa madhehebu ya Shia nchini humo.
Disemba mwaka jana 2015, jeshi la serikali ya Nigeria lilishambulia kituo cha kidini cha Waislamu hao na kuua mamia miongoni mwao katika mji wa Zaria. Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na wenzake kadhaa pia wangali wanashikiliwa na vyombo vya usalama kwa miezi kadhaa sasa.
http://parstoday.com/…/africa-i6976-wanaharakati_uingereza_…