IMAM WA MASJID GHADIR KHUM (Kigogo)




Shk: Hemed Jalala

Bismillah Rahmanr Rahiim
SURA YA KWANZA


MAANA YA “SHIA”

Swali:
Nini maana ya neno“Shia?”

Jawabu:
Neno “Shia” linatokana na neno “Mushaayea’t ambalo maana yake ni kufuata.

Swali:
Kwa nini Mashia wanaitwa kwa jina hilo?


Jawabu:
Kwa sababu wanamfuata Sayyidna Ali (a.s) na wazao wake watakatifu wa Mutme Muhammad (s.a.w.w) yaani Ahlul-Bayti.

Swali:
Nani amewapa jina hilo?

Jawabu:
Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndie aliyewapa jina hilo kama ilivyo andikwa katika vitabu vya Kisunni na Kishia.

Swali:
Mashia wangapi wako duniani?Jawabu: Zaidi ya milioni mia mbili (200,000,000).

Swali:
Wanaishi katika nchi gani?

Jawabu:
Maisha wametawanyika katika kila nchi ya kiislaam na isiyokuwa na Kiislaam, na wengi wao wako nchini Iraq, Iran, Lebanon, India, Pakistani, Indonesia, Afghanistan, Turkey, Umoja wa falme za Kiiarabu, Oman, Kuwait, Bahrain, Afrika ya mashariki n.k.


Swali:
Je wanayo serikali yao wenyewe?


Jawabu:
Ndio, nayo ni serikali ya Iran.

Swali:
Je, walikuwa nazo tawala zao hapo zamani?

Jawabu:
Ndio, tawala nyingi walikuwa nazo, kwa mfano, tawala za Safawiyya, Buwayhiyyah, Idrisi, Hamdani, Qajar, Fatimiy,n.k.


Swali:
Mashia wanao maulamaa (wanavyuoni wa dini)?

Jawabu:
Ndio, wako wengi kama nyota, tangu zamani hadi sasa.
 

Swali: Je, Mashia wanavyo vitabu vilivyopigwa chapa yao wenyewe?


Jawabu: Ndio, tena idadi ya vitabu hivyo ni kama mchanga.

Swali:
Je, Mashia wanayo adabu njema ya kuishi pamoja na Waislaam wengine kwa udugu, mapenzi na ushirikiano?


Jawabu:
Ndio, mifano ya maisha yao inaweza kuonekana kila mahala, pawe Baghadad, Misri, Damascuas au Beirut, n.k. Mashia Na Masunni wanaishi pamoja kama ndugu.

Swali:
Je, Mashia wanayo madarasa (Vyuo vya dini) zao wenyewe?

Jawabu:
Ndio, kuna madarasa nyingi, hususan katika miji ya Najaf, Karbalaa, Kadhimain Samarrah, Qum, Mash’had, Tehran, Isfahan, Beirut, Shiraz, Damascus,Tanzania, n.k.

Swali:
Eti Mashia huwahesabu Waislaam wengine kuwa ni makafiri?

Jawabu:
Huu ni uzushi na uwongo usio na msingi ulio buniwa na wafitini.

Swali:
Je, ni kweli kuwa wao huwaita masahaba wa Mtume mtukufu “makafiri” na huwalaani?

Jawabu:
Huu pia ni uzushi uwongo unaoenezwa na wale ambao wanataka kuleta ugomvi.

Swali:
Je, ni kweli kuwa wao huyasujudia masanamu?

Jawabu:
Huu ni uwongo na tuhuma tu. Inaruhusiwa kusujudu juu ya ardhi tu, au juu ya kile kinachoota humo ikiwa tu hakiliwi au hakivaliwi.

Swali:
Katika miji gani zipo madarasa na wanavyuoni wengi, lakini inayojulikana sana ni miji ya Najaf, Karbala, Qum, na Mashhad.

Swali:
Wapi mtu anaweza kupata maelezo kamili na sahihi juu ya itikadi za kishia?

Jawabu:
Unaweza kupata katika Mtandao wetu huu wa www.afroshia.blogspot.com, au tuandikie katika barua pepe: afroshiatz@gmail.com, hemedijalala@yahoo.com pia unaweza kupata maelezo zaidi kwenye namba hii ya simu, +255 715 936545.

AU TEMEBELEA MAKTABA ZETU MBALIMBALI KAMA IFUATAVYO:-
Imam Swaadiq (Kigogo Post kwa Shk Hemed Jalala), Magomeni Mzimuni (Shk Ali J. Mayunga), Magomeni Mapipa Mtaa wa Kisiju (Shk Musabah S. Mapinda), Kinondoni Mtaa wa Kumbukumbu (Shk Waziri O. Nyello), Masjid Imam Ali Bin Abi Talib Lushoto,Tanga(Shk Baqiir Mwenda), Masjid(Madrasa Imam Mahd)(Shk Twahiir Abdallah), Yombo (Shk Ridhiwan Pingili)

Swali:
Kwa nini Mashia wanaitwa ja’fari?

Jibu:
Kwa sababu Imamu wa sita Ja’afar Sadiq (a.s) alieneza kwa wingi sana mafundisho ya Qur’an na Mtukufu Mtume (s.a.w.w), hata kwamba hadithi nyingi (zinazopatikana katika Shia), tafsir, Fiqh na maarifa mengineyo yanatoka kwake.

SURA YA PILI

ITIKADI YA KISHIA

Swali:
Nini itikadi ya Mashia?

Jawabu:
Mashia wanaamini Misingi Mitatu.

Swali:
Misingi ipi hiyo?

Jawabu:
Misingi yenyewe ni hii:

1-
Muumba na sifa zake;

2-
Utume na mambo yanayo husiana nao,

3-
Kiyama na mambo yanayopatikana humo.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Muumba?

Jawabu:
Mashia wanaamini kuwepo kwa Mungu mmoja, Mwumba wa ulimwengu, mwenye kuruzukum mwenye kuhuisha, Mjuzi, Muweza, Hai, Mdiriki, Mwenyeenzi, Asiye na Mwanzo wala Mwisho, Msemi, Mkweli, Asiye na mwili, Asiyeonekana, Asiyebadilika. Asiye na mshirika, Naye ni mwadilifu katika vitendo, maamrisho na uumbaji, kama anavyosema Mwenyewe katika Qur’an: “hakika mola wako si dhalim kwa waja wake”. (Qur’an,3:181).

Swali:
Nini itikadi ya Maisha juu ya Utume?

Jibu:
Mashia wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu amewatuma mitume na manabii kuwaongoza wanadamu kutoka katika upotovu na ujinga na kuwaita katika njia ya uongofu wa ukweli. Hao mitume walikuwa wengi sana, miongoni mwao ni Muhammad (s.a.w.w) Mtume wa Uislaam. Vilevile manabii Musa, Isa, Nuh, Ibrahim (amani iwe juu yao) na manabii wengine, wametajwa katika Qur’an na hadithi. Hao wote hawakuwa na dhambi na walitumwa na Mwenyezi Mungu kufikisha ujumbe uliokamilika na usio na upungufu wa mola wao.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Uimamu?
 

Jibu: Mashia wanaamini kwamba Mtume mtukufu (s.a.w.w) aliwachagua Makhalifa (maimamu) Ithna asharia (12) kwa amri ya Mwenyezi Mungu na akawataja kwa majina yao. Wao wamehifadhika kutokana na kila dhambi na makosa kama Mtume mtukufu (s.a.w.w) alivyo, ambaye kwa ajili ya sifa zake Mwenyezi Mungu amesema: “Hasemi kwa matamanio yake, ila tu ni Wahyi (Ufunuo) uliofunuliwa”. (Qur’an, 53: 3).


Swali: Ni nani hao Maimamu na Makhalifa wa Mtume?

Jibu:
Wao ni:

1-Ali Amirul Mu’miniin

2-Hassan

3-Hussein

4-Ali bin Huseyni

5-Muhammad Baqir,

6-Ja’far Sadiq

7-Musa Kaadhim,

8-Ali Ridha,

9-Muhammad Taqi,

10-Ali naqi,

11-Hassan Askariy, na

12-Muhammad Mahdi (amani iwe juu yao).

Majina yao na ukhalifa wao vimeandikwa kufuatana na hadithi za Mtume katika vitabu vya kisunni na vya kishia pia.

Swali:
Hao Maimamu wamezikwa wapi?

Jibu:
Ali (a.s) amezikwa mjini najaf (nchini Iraq); Hassan, Ali bin Husein, Muhammad Baaqir na Ja’far Sadiq (a.s) wamezikwa madina (nchini Saudi Arabia); Husein (a.s) amezikwa Karbalaa (nchini Iraq); Musa Kadhim na Muhammad Taqi (a.s) wamezikwa Kaadhimaini (nchini Iraq); Ali Ridha (a.s) amezikwa Mashhad (nchini Iran); Ali Naqi (a.s) na Hassa Askariy mjini Samarrah (nchini Iraq).

Swali:
Je, makaburi ya Maimamu (a.s) hao yapo hadi hivi sasa?

Jibu:
Ndio, Waislaam wameyajengea makaburi ya Maimamu (a.s) majengo makubwa, na maelfu ya Waislaam kutoka kote duniani huyazuru kila mwaka kama kuonyesha heshima yao.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Imamu Mahdi (a.s).ibu: Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amebashiri kwamba Imamu Mahdi (a.s) atabaki hai hadi atakapodhihiri baada ya muda mrefu wa kughibu (kutoonekana) kwake, ili kuleta uadilifu na amani duniani baada ya kuwepo dhuluma na maonevu, kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Kisunni na Kishia.

Swali:
Je, ni kweli kwamba Mashia wanavuka mpaka kwa kuwasifu Maimamu?

Jibu:
Si kweli kabisa! Wao wanaitakidi kuwa hao Maimamu walikuwa waja wanyenyekevu wa Mwenyezi Mungu, na Makhalifa wa Mtume wake (s.a.w.w).

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Bibi Fatimah Zahraa, binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)?

Jibu:
Wao wanaitakidi kuwa yeye ni Mkweli (Siddiqah) na Johari (RTTaahirah); na Mwenyezi Mungu ameteremsha aya ya Tat-hir kwa utukufu wake, na baba yake, na wa mume wake, na wa wanawe.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Qur’ani?

Jibu:
Mashia wanaamini kwamba Qur’ani ni Neno la Mungu, ambalo alimteremshia Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) kuwa mwujiza na mwongozo, nayo ni kitabu chenye ukweli kisichokuwa na uwongo ndani yake, pia ni msingi wa sheria zote, kisicho ongezwa wala kupunguzwa maneno yoyote yale.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya Uislaam?

Jibu:
Mashia wanaamini kwamba Uislaam ni dini iliyofundishwa na manabii na mitume wote, ambayo mafundisho yake yalikamilishwa na Mtume wa Uislaam-Muhammad (s.a.w.w). Dini hii itaendelea kuwepo mpaka siku ya Kiama, “Na mwenye kufuata dini isiyokuwa ya Uislaam, basi haitokubaliwa kwake, na (siku ya) akhera atakuwa miongoni mwa waliopata hasara”. (Qur’an, 3:84).

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya majaaliwa?ibu: Mashia wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu Amemwumba mwanadamu akiwa na uwezo tofauti: Amwmwongoza katika mema na kumfungulia njia zote. Basi yule mwenye kuasi na kukufuru huwa amejifanyia mwenyewe; na mwenye kuamini, akaongoka na akatii basi huwa ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kwa ubora wa hiari yake; kama ilivyoelezwa katika hadithi inavyosema: “Hakuna jambo la kulazimishwa au la uhuru kabisa ila lipo jambo moja kati ya hayo mawili”

Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya “Taqiyyah” (kutodhihirisha imani?
Jibu: Itikadi ya Kishia juu ya “Taqiyyah” inaelezwa katika Qur’ani Tukufu na Mwenyezi Mungu: “Anayemkataa Mwenyezi Mungu baada ya imani yake, isipokuwa yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani…” (Qur’ani, 16:106). Vilevile anasema “Walioamini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi badala ya wanaoamini, na atakayefanya hivyo, basi hatakuwa na chochote kwa Mwenyezi Mungu, ila ya kwamba mjilinde na maovu yao…” Qur’ani, 3:28). Mwislaam anatakiwa ayashike maamrisho ya kiislaam lakini hata hivyo anaweza kwenda kinyume chake (kwa kutodhirisha) katika wakati wa hatari na mashaka, kama anavyosema Mwenyezi Mungu: “Mwenyezi Mungu Huwatakieni yaliyo mepesi wala Hawatakieni yaliyo mazito” (Qur’ani, 2:78) Pia Mtume Mtukufu amesema: “Hakuna madhara wala shida katika Uislaam”.


Swali:
Nini itikadi ya Mashia juu ya ukafiri na Uislaam?

Jibu:
Mashia wanaamini kwamba Mwislaam ni yule ambaye anashuhudia shahada mbili, “ Hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad ni Mtume wake”. Isitoshe, anafuata maamrisho yaliyoletwa na Mtume ZMtukufu (s.a.w.w) kutoka kwa Mola wake. Mtu huyu anastahiki kupewa hifadhi ya nafsi yake, mali na heshima yake na huwa ametakasika. Mambo yanayo wahusu Waislaam yanamhusu yeye pia, vilevile mambo yake yanawahusu Waislaam wote. Kafiri ni yule anayekataa shahada yoyote kati ya hizi mbili, au anakataa jambo lolote katika mambo ya kiislaam ambalo linajulikana kuwa ni miongoni mwa mafundisho ya Mtume (s.a.w.w).

Swali:
Nini maana ya “Usmat”

Jibu:
“Ismat” (Umaaasumu) maana yake ni kutakasika kabisa kutokana na kila dhambi na dosari iwe ndogo au kubwa.

Swali:
Ni nani Maasumu (alie takasika na dhambi) kufuatana na itikadi ya Kishia?

Jibu:
Waliokuwa Maasumu ni Mitume, Manabii, Maimamu, Bibi Fatimah binti wa Mtume na Malaika, kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuhusu Malaika: “ Hawamwasi Mwenyezi Mungu kwa anayowaamrisha, na wanafanya kama wanavyoamuriwa”. (Qur’ani, 66:6)Swali: Nini itikadi na maelezo ya Mashia juu ya Kiyama?

Jibu:
Mashia wanaamini kwamba mtu anapotokwa na roho haangamii kama wanavyosema walahidi. Walikini anahamishwa kutoka dunia hii na kupelekwa katika dunia nyingine iitwayo Barzakhi. Hakika kaburi ni bustani katika mabustani ya Peponi kwa mwenye kuamini; na ni shimo la moto katika mashimo ya Motoni kwa mwenye kukufuru na kuasi. Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama atafufua maiti za wote wawili ili kuhesabu vitendo vyao. Yeye aliyekuwa mwema atalipwa kwa kuwekwa katika mabustani ya neema, na yule aliyekuwa mwasiatatupwa katika shimo la Moto. Siku hiyo kutakuwako sirati, Mizani, Kitabu Hodhi, Bustani na Moto.

Swali:
Nini itikadi ya Mashia kuhusu “Shifaa” (Maombezi)?

Jibu:
Mashia wanaitakidi kwamba Mwenyezi Mungu atamruhusu yule amtakaye miongoni mwa Manabii, Maimamu, Maulamaa, na Mashahidi, na watu wema na kadhalika kuwaombea (kuwashafiia) baadhi ya waliotenda dhambi-kama anavyosema katika Qur’ani: “Hawata waombea ila yule aliyemridhia”. (Qur’ani, 21:28) Na Mtume Mtukufu (s.a.w.w)amesema: “Shifaa yangu itakuwa kwa wale wafuasi wangu waliokuwa na madhambi”.

SURA YA TATU

IBADA ZA KISHIA

Swali:
Mashia wanafanya ibada gani?

Jibu:
Ibada za Kishia ni zile zile kama walivyoamuriwa na Mtumufu Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) nazo ni: utwahara, sala,zala,kufunga, kudhikiri, hija, jihadi, khumsi, kuamrisha mema na kukataza maovu.


Swali:
Je, kuna tofauti yoyote katika misingi ya ibada za Kishia na Kisunni?

Jibu:
Hakuna tofauti katika misingi ya ibada za Kishia na KIsunni; Lakini kuna tofauti katika mambo ya hukumu za sheria (Masaailil-fiqhiyyah) kama ilivyo tofauti hizo kati ya madhehebu za Hanafii, Shafii, Hambali na Maliki.

Swali:
Je, Mashia wanazitii na kuzitekeleza ibada hizo?

Jibu:
Mashia ni Waislaam wa dhati katika kutii na kutekeleza ibada. Wanayo misikiti mingi mikubwa ambamo humo hukusanyika kila siku nyakati tatu kusali sala ya jamaa. Nyakati za sala huadhiniwa adhana na ikama. Hufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kila mwaka, ibada kubwa ya wale Mashia walio na uwezo huenda kuhiji kuliko Waislaam wengine ukilinganisha na idadi yao. Pia hutoa malipo ya khumsi na zaka kwa wingi, jambo ambalo huwasaidia maulamaa kuendeleza kazi za kidini pasina kuhitaji msaada wa serikali. Malipo hayo hutumika kuwasaidia Mashia maskini, kuendesha vyuo vya kidini, misikiti, upigaji chapa, kueneza dini, kuimarisha madarasa ya kuhifadhi Qur’ani kwa moyo, na kadha wa kadha. Ama kuhusu Jihadi (vita vya kidini), Mashia wanasifika katika kujitolea kwao. Wamepigana Jihadi vyema, hususani dhidi ya wakoloni waliovamia madola ya kiislaamu baada ya kuanguka kwao, jambo ambalo liliwafanya wasisite kujitolea kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Uislaam. Historia inaeleza juu ya ukweli huu. Mashia kwa hima wanawaamrisha, watu kutenda mema na kuwakataza kutenda maovu. Wanajitahidi usiku na mchana katika kazi hii, kwa kuhubiri juu ya mimbari na kwa kuandika vitabu, jambo ambalo wameta fora. Mbali na hayo, Mashia pia husali sala za sunna, hufunga saumu za sunna, na hutekeleza ibada zingine kama kutoa sadaka na wakfu, kudhikiri, kusaidia katika mambo ya kidini na kutii maamrisho yote.

SURA YA NNE

SHERIA ZA KIISLAAMU

Swali:
Nini sheria za Kishia kuhusu mambo na maamrisho ya Kiislaam?

Jibu:
Tofauti zilizopo kati ya Ushia na Usunni katika mambo ya sheria na maamrisho ya dini ni sawa na tofauti zilizopo kati ya madhehebu za Kisunni katika sheria za ununuzi, uuzaji, rehani, kazi, ndoa, talaka, kilimo, fedha, deni, mkopo, eda, uwindaji, dhabihu, kula, kunywa, ardhi, hukumu, ushahidi, malipo, kisasi na kadhaa wa kadha. Hukumu juu ya mambo haya yote yanategemewa kupatikana katika Qur’ani na Sunna tu, wala hairuhusiwi kutegemewa kupatikana kutoka mbali na vitu hivi viwili.

Swali:
Je, Ushia unaruhusu kufunga ndoa ya muda maalum (Mut’ah)?

Jibu:
Ndiyo, inaruhusu. Kuna thibitisho katika Qur’ani na Sunna juu ya jambo hili, kama ilivyoelezwa kwa urefu katika kitabu cha Mut’ah.

Swali:
Nini maoni ya Mashia kuhusu zama hii ya kisasa ambayo mambo mengi yanabadilika kufuatana na wakati ulivyo?

Jibu:
Kufuatana na maoni ya Mashia, Uilsaam si dini isiyokamilika, hata ikahitaji mabadiliko ya Sheria na maamrisho yake kwa sababu ya kubadilika kwa wakati na mazingira ya Mashariki na magharibi. Kwa kweli, sheria za kiislaam zimefanywa ili kuweza kufaa na kutumika katika kila zama, mazingira, jamii na kizazi. Uislaam ni dini yenye sheria kamili ambayo haihitaji sheria nyingine. Sheria za kiislaam zimewekwa kwa nidhamu na utaratibu kufuatana na hali mwanadamu tangu anapozaliwa hadi anapokufa ili aweze kufaa na kutekelezeka katika mambo ya uchumi, siasa, jamii, tabia, biashara, kilimo, viwanda, ujenzi, uchimbaji wa madini, misafara ya baharini na angani, shughuli za kinyumbani, elimu, utafiti, vita, amani, mikataba ya serikali, n.k. Ikiwa mataifa ya dunia yatafuata sheria za Kiislaam katika mambo yao yote, basi yatajipatia maendeleo makubwa. Vitabu vingi vinapatikana kila mahala vilivyoandikwa na Mashia vikuhusiana na mambo haya juu ya maisha ya kisasa na sheria za kiislaam. Vitabu hivyo vinathibitisha kwamba sheria za kiislaam zinaweza kufaa na kutumika katika mambo yote ya maisha kama Mwenyezi Mungu alivyoamuru na kuelezwa na Mtume Mtukufu (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) na kama ilivyotajwa katika Qur’ani na Hadithi.

SURA YA TANO

MEMA NA MAOVU

Swali:
Ni mabo yapi yaliyo mema na yapi yaliyo maovu kwa Mashia?

Jibu:
Mambo mema ni yale yenye sifa njema na vitendo vizuri ambavyo Uislaam unawalazimisha wafuasi wake kuyafanya daima, na mambo maovu ni kinyume cha hayo. Haya ni mema: Ukweli, uaminifu, udhati, upole, uwastani, ushujaa, ukarimu, heshima, uadilifu, ucha Mungu, uvumilivu, kutosheka, unadhifu, kuwatazama wazazi, elimu, subira, ustahmilivu, udugu, unyenyekevu, adabu njema, maneno mazuri, kusamehe, mapenzi, upatanishaji uongozaji, hisani, kuwasaidia wahitaji na kadha wa kadha.

Haya ni maovu: 

Uwongo, hiana, ubakhili, woga, kupuuza, kuvunja miadi, dhuluma, uchafu, ujinga, pupa, uroho, majivuno, kutowatii wazazi, kuudhi, kushambulia, uasherati, fitina, kusengenya, chuki, wizi na kadhaa wa kadha.