Bismillahir Rahmanir Rahim.
Tarehe ishirini na nane, mwezi wa mfungo tano mwaka wa kumi Hijiria, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifishwa. Mara baada ya kufariki Bwana Mtume (s.a.w.w) Maswahaba wengi walikwenda katika ukumbi wa Bani Saaidah, kufanya kampeni ya kumchagua atakayeshika mahala pa Bwana Mtume, hatimae wakamchagua Abubakar bin Abi Quhafa. Kisha Abubakar bin Abi Quhafa alimpeleka Umar bin Khattab nyumbani kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s), na alipofika akawaita waliokuwa ndani ya nyumba ya Imam Ali bin Abi Talib (a.s) lakini wakakataa kutoka. Ndipo Umar bin Khattab alipoagiza ukuni wenye moto na akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi ya Umar bin Khattab iko katika milki yake, lazima mtatoka, au Wallahi nitawaunguza wote mliomo humo. Akaambiwa: "Ewe baba Hafsa! humo mna Fatma. Akajibu: Japo. Kisha Umar bin Khattab akasimama akiwa na kundi la watu, wakagonga mlango. Mwana Fatma aliposikia sauti zao, akaita kwa sauti ya juu; "Ewe baba! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jambo gani linatufika baada yako, kutoka kwa Umar bin Khattab na kwa Abubakar bin Abi Quhafa?" Jamaa walipoisikia sauti ya Bibi Fatma (a.s) akilia na kuita hivyo, baadhi yao waliondoka wakilia sana. Na wengine wakabaki na Umar bin Khattab ambao walimtoa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) na kumpeleka kwa Abubakar bin Abi Quhafa, kisha wakamwambia: "Mpe baia. Imam Ali akakataa. Wakasema: "Kwa hiyo wallahi tutakata Shingo yako. Imam Ali bin Abi Talib (a.s) akawauliza: "Mnamuua Mja wa Mwenyezi Mungu na ndugu ya Mtume wake? Umar bin Khattab akasema: "Ama Mja wa Mwenyezi Mungu ni sawa, ama ndugu ya Mtume wake si sawa. Na Abubakar bin Abi Quhafa yupo kakaa anaangalia. Umar bin Khattab akamuuliza Abubakar bin Abi Quhafa: Nimfanye nini? Abubakar bin Abi Quhafa akajibu simlazimishi chochote mazali Fatma yuko naye. Kisha Imam Ali bin Abi Talib (a.s) alikwenda katika kaburi la Bwana Mtume (s.a.w.w) akalia na huku akiita: "Ewe ndugu yangu! Hakika watu wamenidhalilisha na wamekaribia kuniua!"
Taz: Al- Imama Wassiyasa J.1 Uk. 39 - 31
Katika ukumbi wa Bani Saaidah walijumuika Muhajir na Ansar tayari kwa uchaguzi. Abubakar alitoa Khutuba ndefu akiwakumbusha kwamba: Muhajir ndio walio na haki ya kushika uongozi mahala pa Bwana Mtume (s.a.w.w) Khutuba ambayo ilijibiwa baadae na Hubab bin Mundhir katika Ansaar. Naye akionyesha kuwa Ansaar ndio walio na haki ya kushika uongozi mahala pa Bwana Mtume (s.a.w.w) na ikiwa hapana budi, basi kwa Muhajir atoe mmoja na kwa Ansaar atoke mmoja. Ndipo Umar bin Khattab aliposimama akasema: "Hilo haliwezekani, panga mbili hazikai katika ala moja, Wallahi Waarabu hawakubali kuwatawalisheni na hali Mtume wao hatokani nanyi."
Saad bin Ubada, mkuu wa taifa la Khazraj, alipotakiwa kumbai Abubakar bin Abi Quhafa akakataa akasema: "Wallahi nitakupigeni mishale yangu yote na mikuki yangu kwa kadiri ya uwezo nilionao, nitakupigeni pamoja na watu wa nyumbani kwangu na wanaonitii katika kaumu yangu, Wallahi lau Majini watakukusanyikieni pamoja na watu wote sitokupeni baia, mpaka nitakufa niende kwa Mola wangu na nijue hesabu yangu."
Umar bin Khattab anasema: " Kwa kweli kuchaguliwa kwa Abubakar kulitokea ghafla, na Mwenyezi Mungu aliepusha shari yake."
Taz: Tarekhu Ibn Athir J.2 Uk. 220 - 225
Tarekhut Tabari J.2 Uk. 458 - 459
Imepokewa kutoka kwa Urwa kuwa: "Abubakar na Umar hawakuwapo katika mazishi ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w). Walikuwa katika ukumbi wa Bani Saaidah wakishughulika na kampeni ya Uchaguzi.
Taz: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652
Abubakar bin Abi Quhafa anasema: "Hakika mimi sijuti juu ya jambo lolote katika dunia hii ila..... nilipenda siku ya Saqifa bani Saaidah, mimi ningelitupa jambo hili kwa mmoja wa watu wawili, Umar bin Khattab au Abu Ubaida bin Jarrahi, mmoja wao awe awe Amir nami niwe Waziri."
Taz: Kanzul Ummal J.5 Uk. 632
Tarekhut Tabari J.2 Uk. 619