Hivi karibuni wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul Bayt (a.s) kutoka Mikoa
mbalimbali nchini Tanzania walifanya Ziara katika Mkoa wa Kagera Wilaya
ya Muleba, Ziara ambayo ilijumuisha wasomi wa kike na wa kiume wa dini
ya Kiislam, msafara huo Mtukufu ulipokelewa na ndugu Gataya Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Mashia Ithna Ashariyyah Mkoa wa Kagera, msafara huo
ulitembelea vituo vya watoto yatima eneo la Kashai na Mghembe pia
walipata bahati ya kuitembelea familia iliyoingia katika dini ya Kiislamu
na kufikisha salamu kutoka kwa ndugu zao Waislamu baada ya hapo msafara
huo ulifika katika Msikiti wa Ijumaa uliyochini ya Bakwata (Jaamiah)
ambapo walitoa Mawaidha kwa Waislamu na jioni yake walimalizia kazi yao
kwa kufanya Majilisi ya vitendo pamoja na Wanafunzi wa Hawza.
Baadhi ya washiriki wa msafara huo wamepongeza sana jitihada kubwa zilizofanywa na jamii ya Mashia kwa kutoa michango yao kwa nia nzuri katika kufanikisha safari hiyo iliyogharimu kiasi cha zaidi ya Milioni moja wamesema inapendeza kwa kiasi kikubwa inavutia na kutia moyo na inaonyesha ni jinsi gani mafanikio yanavyopatikana katika Mashia wa Afrika Mashariki, Miaka kadhaa iliyopita hadi kufikia juzi na jana kulikuwa hakuna anayeweza kufikiria Mwafrika anaweza kuwa sikio la wanyonge leo hii Mwafrika anaweza kutoa Shilingi yake kwa Moyo mmoja kwa ajili ya kueneza Uislamu halisi wa Mtume (s.a.w.w) mara zote watu waliwezeshwa kutumwa kwa malipo ili kutoa Majilisi na kupumbazwa na kuona mafanikio ya Tabligh haya wezi kwenda bila kusimamiwa au kudhaminiwa lakini leo Mwafrika ana hama anajitambua anazinduka anaamka na kuonesha kuwa anaweza kufanya kitu kikubwa zaidi ya Tabligh ya mara moja kwa mwaka au Mkoa mmoja kwa mwaka bali Afrika Mashariki yote inawezekana kufikia kwa umoja na Mshikamano na Ikhlaswi.