Wanaharakati na wapenda haki ulimwenguni wameadhimisha kumbukumbu ya Alfajiri kumi. Tarehe Mosi Februari inasadifiana na siku aliyorejea nchini Iran Imam Khomein MA akitokea uhamishoni nchini Ufaransa. Kurejea Imam Khomein nchini Iran kuliongeza kasi ya Mapambano ya wananchi ya kuuondoa madarakani utawala wa Kitwaghuti wa Shah. Siku kumi baada ya kurejea Imam Ruhullah Khomein MA, Mapinduzi ya Kiislam yalipata ushindi, na kipindi hicho cha siku kumi za baina ya kurejea Imam hadi kupata ushindi kamili Mapinduzi ya Kiislamu, kinajulikan Iran kwa jina la "Alfajiri kumi". Licha ya kuweko njama za Mabeberu za kila upande dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini Mapinduzi haya Matukufu yameweza kudumu na kupata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali.