IMAM KHOMEIN (R.A) alikutana na wahitimu wa masomo ya juu ya dini Najaf Al-Ashraf na kuwahutubia. Hotuba ambayo ilifanywa kuwa kitabu: "Alhukuumatul Islaamiyya" katika ukurasa wa ishirini (20) , Imam alisema: "Ni juu yenu kuutangaza Uislamu kama unavyotakikana kutangazwa. Wajulisheni watu Uimamu kama ulivyo, waambieni kuwa: Sisi tunaamini Uimamu, na kwamba: Mtume (s.a.w.w) aliuweka kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na tunaamini vilevile haja ya kuunda Serikali. Tunajitahidi kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na hukumu yake, na kwa ajili ya kuongoza watu na kuwasimamia na kuwaangalia. Lamuhimu ni kuunda Serikali iliyo sambamba Imani na Uimamu. Andikeni na msambaze misingi ya Uislamu wala msiifiche wajibikeni nyinyi wenyewe kutenda hukumu ya Kiislamu na mjitegemee wenyewe na muwe na hakika ya kushinda. Wakoloni zaidi ya karne tatu kabla, walijiandaa wenyewe, na wakaanza mwanzo kabisa na sifuri, baadae wakapata waliyoyakusudia. Nasi tuanze hivi sasa kutoka sifuri. Msiwape nafasi (kuongoza) watu wa Magharibi na wafuasi wao kuliko nyinyi wenyewe. Wajulisheni watu ukweli wa Uislamu, ili jamii ya vijana wasifikiri kuwa: Wenye elimu walioko katika vyuo vya Najaf na Qum wanaamini kuwa Dini na siasa ni vitu viwili mbalimbali, na kwamba wao hawashughuliki na jambo lolote isipokuwa somo la hedhi na nifasi tu, wala hawana habari na siasa."
Hili ndio agizo la Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Agizo ambalo linawataka Waislamu wote ulimwenguni kuwa wakweli juu ya dini yao.
Hili ndio agizo la Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Agizo ambalo linawataka Waislamu wote ulimwenguni kuwa wakweli juu ya dini yao.