IRAN IMEADHIMISHA SIKU YA MAPINDUZI YA KIISLAM.

Maandamo makubwa yafanyika leo hii Qom Iran kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Kiislam. Imam Khomeini (r.a) siku aliporejea nchini Iran akitokea uhamishoni Ufaransa mnamo tarehe Mosi Februari kuliongeza kasi ya mapambano ya wananchi ya kuuondoa madarakani utawala wa kitwaghuti wa Shah. Siku kumi baada ya kurejea nchini Imam Ruhullah Khomeini MA, Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi, na kipindi hicho cha siku kumi za baina ya kurejea Imam hadi kupata ushindi kamili Mapinduzi ya Kiislamu, kinajulikana nchini Iran kwa jina la "Alfajiri Kumi". Licha ya kuweko njama za mabeberu za kila upande dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini mapinduzi haya matukufu yameweza kudumu na kupata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Khamenei, yoyote atakayetaka kulidhalilisha taifa la Iran atakabiliwa na jibu la kudhalilisha pia.