Imam Hussein (a.s) aliona kwamba watu wameicha njia iliyoonyoka kwao na Mtukufu Babu yake (s.a.w.w) na wazazi wake, watu wameanza kujipatia tu na kuchukua kutoka kwenye dini na maadili haya ya Kimungu, kiutu na ya Ki-Qur'an ya Infaq yalikuwa yanauawa na watu sawa tu kama maadili mengine. Watu wameondoa nafsi katika maadili haya ya kutoa katika njia ya Allah na yamebadilishwa na uovu (Munkar). Haichukui muda mrefu kwa maadili kubadilika, kwa muda wa miaka hamsini na moja tangu kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w), maadili yote yamebadilika. Uhusiano wa watu umebadilika kutoka kwenye kutoa na kuwa wa pato, na uhusiano huu wa kila siku kupata na kuchukua kutoka kwenye dini ulikuwa ukihesabiwa kama maadili.
Kiongozi wa Mashahidi aliwasilisha ufafanuzi wa kimatendo wa Infaq katika Karbala. Imam Hussein (a.s) aliwasilisha ufafanuzi wa kimatendo wa Aya hii ya kutoa katika njia ya Allah katika hali ambayo alitumia aina zote za riziki alizokuwa nazo katika hadhara ya Allah (s), na alitoa riziki hizo katika hali ambayo haikubakiwa na kitu. Imam Hussein (a.s) aliwasilisha ujuzi wake katika njia ya Allah, alifanya kitendo cha kutoa katika njia ya Allah kutokana na mwongozo wake, aliendelea kutoa Khutba ili kuwafanya watu wale maaluni waelewe na kuwaleta kwenye njia iliyonyooka, kisha baada ya hili aliwasilisha mali yote aliyokuwa nayo katika njia ya Allah (s). Mke wake, Hadhi yake, Watoto wake, Masahaba zake, kila kitu kilitolewa Muhanga kwa ajili ya kutoa katika njia ya Allah (s).
Ni lini utapata watu wakarimu kama hawa? Watu wanatoa mfano wa Hatim Tai kama mtu mkarimu sana, ingawa Hatim Tai mkarimu alikuwa na uwezo tu wa kulisha watu masikini kutoka kwenye utajiri wake. Lakini, ni Karbala iliyoonesha na kutuambia kuhusu watu wakarimu mno katika ulimwengu huu.
Jina la mtu mkarimu mno katika ulimwengu huu ni Hussein (a.s). Chochote alichokuwa nacho, alikiwasilisha kwa Allah kimoja baada ya kingine. Mtu huyu Mashuhuri wa Infaq alipita katika hali fulani wakati alipokuwa ametumia riziki yote aliyokuwa nayo katika njia ya Allah, alirudi kambini na kwenye mahema yake kuona kama kuna riziki yoyote iliyobakia. Alikwenda kwenye hema ya Masahaba zake na kuona kwamba riziki ya Masahaba yote ilikuwa imekwisha; kila kitu kilikuwa kimetumika katika njia ya Allah. Aliona kwamba hema la Abbas (a.s) lilikuwa tupu kwa vile riziki hii ya Ali (a.s) vilevile ilikuwa imetumika katika njia ya Allah. Aliingia ndani ya hema la Ali Akbar (a.s) na akaona kwamba riziki hii pia imetumika katika njia ya Allah. Wakati alipokuwa ameachwa peke yake kabisa, alirudi kwenye uwanja wa Mapambano na kuanza kuwaita Masahaba zake kwa sauti ya juu. Aliangalia kushoto na kulia, lakini hakuona Sahaba yeyote; wote walikuwa wamepumzika kwenye ardhi ile inayochoma ya Karbala. Yeye (a.s) akawaita kwa sauti ya juu na kusema: "Ewe Muslim bin Aqil, Ewe Hani bin Urwah, Ewe Habib bin Mazahir, Ewe Zuhair bin Qain..... Enyi watu waaminifu! Enyi watu wenye ari! Enyi watu mliojitayarisha kwenda kwa ajili ya mapambano! Ni nini kilichowatokea? Nawapigieni ukelele wa kuwaita, lakini hamjibu, je, mmekwenda kulala? Ninayo matumaini kwamba mtaamka, au ahadi yenu ya utii na Imam wenu imekwisha na ndio maana hamnisaidii? Hawa ni Mabinti wa Mjumbe wa Allah (s.a.w.w), Enyi Mabwana wa upole! Nyanyukeni kutoka kwenye usingizi wenu mzito ili muwahifadhi Harem (Wanawake) wa Mjumbe wa Allah (s.aw.w) kutokana na wachupa mipaka hawa waliolaaniwa."
Rejea: (Mawassae Kalemate Imam Hussein - Uk. 484)
Nyoyo zangu shujaa, Simba zangu! Mko wapi? Askari wangu mashujaa! Mko wapi? Kwa nini hamuamki kutoka kwenye usingizi wenu mtamu, amkeni? Watupeni maaluni hawa mbali na Harem (Wanawake) wa Mjumbe wa Allah (s), amkeni! Wakingeni Ahlul Bayt (a.s). Wakati hakuna jibu linalokuja, yeye (a.s) alishawishika kwamba sasa hakuna punje hata moja ya riziki iliyobakia. Ghafla Hussein ibn Ali (a.s) alikuja na kumuuliza Bibi Rubab (a.s) ampe riziki hii ya Allah (s), kwa vile alikuwa anataka kuiwakilisha kwa Allah (s). Hivyo alimuwasilisha kijana huyu vilevile mwenye umri wa miezi sita Ali Asghar (a.s) katika njia ya Allah (s).