IRAN HAIBABAISHWI NA VITISHO VYA MAREKANI.

Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran amesema kuwa, ujumbe muhimu wa Mamilioni ya wananchi wa Iran waliojitokeza kwenye maandamano ya kuadhimisha miaka 36 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini Iran, ni Izza, utukufu na kutosalimu amri mbele ya madola ya kibeberu ya Magharibi. Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami ameongeza kuwa, kujitolea, uaminifu, umoja na mshikamano kati ya wananchi wa Iran ni sehemu nyingine ya ujumbe wa wananchi wa Iran walioshiriki kwa Mamilioni kwenye maadhimisho hayo. Ayatullah Khatami amebainisha kwamba, yapo baadhi ya mapinduzi yaliyojitokeza duniani lakini yalisambaratika baada ya kupita miaka kadhaa, lakini maandamano ya siku ya Jumatano nchini Iran yamewaonyesha walimwengu kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanazidi kupata nguvu na uungaji mkono wa wananchi kila mwaka. Khatibu wa sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kwamba, hadi sasa mapinduzi ya Kiislamu bado hayajachuja na kinyume chake yamekuwa kigezo na kutoa hamasa kubwa kwa baadhi ya nchi nyingine duniani. Ayatullah Khatami ameelezea mwenendo wa mazungumzo ya nyukia kati ya Iran na kundi la 5+1 na kusisitiza kwamba, matamshi ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu yameweza kuzima njama za madola ya Magharibi na hasa Marekani. Ayatullah Khatami amesisitiza kwamba, vitisho na vikwazo vya Wamagharibi kamwe havikuishinikiza Iran iketi kwenye meza ya mazungumzo ya nyuklia, bali azma kuu ya Iran ya kuketi kwenye meza ya mazungumzo na nchi sita zenye nguvu duniani ni kutaka kuuthibitishia ulimwengu kwamba miradi ya nyuklia ya Iran inatekelezwa kwa malengo ya amani.


 

 Chuo Kikuu cha Durban nchini Afrika Kusini kimelaani vikali jinai za kivita zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na kutaka kuchukua maamuzi ya kuwatimua wanafunzi wote wa Kizayuni wanaosoma kwenye chuo hicho. Mkuu wa Kitengo cha Wanachuo katika Chuo Kikuu cha Durban ameeleza kuwa, mwanafunzi yeyote wa Israel ambaye ataonekana akiunga mkono jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina wa eneo la Ukanda wa Ghaza au Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan atafukuzwa chuoni mara moja. Wakati huohuo Baraza la Chuo Kikuu cha Durban kimeomba lisitishwe zoezi la kuwasajili wanafunzi kutoka Israel na kupiga marufuku msaada wa masomo 'scholarship' unaotolewa na utawala wa huo kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na masomo mjini Durban nchini Afrika Kusini. Mara kadhaa mji wa Durban, umekuwa mwenyeji wa mikutano kadhaa ya kimataifa ya kulaani vitendo vya kibaguzi vya utawala wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/46629-chuo-kikuu-cha-durban-kuwa…