Salamun alaykum.
MWALIKO WA KONGAMANO LA KIDINI TAREHE: 17 NA 18 JANUARI' 2015
Taasisi ya Kiislamu ya Imam Bukhary (Imam Bukhary Islamic Foundation)
Inakualika katika Kongamano maalum litakaloshirikisha viongozi mbali mbali wa kidini, wakiwemo Masheikh, Maaskofu, Wachungaji, Maimamu, Waalimu wa Madrasa, watu mashuhuri na waumini mbali mbali, litakalojadili "Madhara ya Misimamo mikali ya imani za kidini (Takfiri) katika jamii na Taifa."
Viongozi kutoka madhehebu mbali mbali ya Kiislamu na Kikristo watatoa
mada na kupendekeza njia za kuzuia Taifa letu kutumbukia katika ghasia
za kidini zinazotokana na kukosekana kwa uvumilivu baina ya wana dini.
Mgeni Rasmi anatazamiwa kuwa Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kongamano litafanyika kwa siku mbili kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 17 -18/1/2015 katika Ukumbi wa Hotel ya Lamada, karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ilala, kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
Chai, na chakula cha mchana vitapatikana.
Wabillahi Taufiq
KAMATI YA MAANDALIZI.
Kwa taarifa yoyote wasiliana na:
Katibu wa Kamati
Jamal Mockry
0713 888 275