Kama
mapungufu ya nuru katika macho ya mtu unaweza kusababisha maumivu ya
tumbo, basi ukosefu wa visheni (uoni) wa jamii utasababisha maumivu na
ufisadi katika jamii nzima. Ukosefu huu wa visheni ni ule wa Umma, hivyo
Imam Hissein (a.s) alisema ninakwenda kurekebisha visheni hii kwa
kuutengeneza Umma. Yazid alikuwa fisadi na uovu wake umefikia kiasi
ambacho hawezi kurekebishwa, lakini tatizo halikuwa
Yazid kama Yazid ilikuwa ni U-Yazid ambao ungekuja kuwepo zama yoyote,
na U-Yazid unaweza tu kuangamizwa kama Umma ungeweza kuwa na uoni wa
kuutambua. Kama Umma haukujenga visheni hii, Yazid ibn Mu'awiya mmoja
atatoweka lakini mtoto wa mtu mwingine atajitokeza kama Yazid. Yazid
huenda anaweza akatokea baada ya miaka elfu moja na mia nne; na kwa hiyo
kazi yangu sio kummaliza Yazid mmoja bali Mayazid wa zama zote. Ni
ufisadi gani uliokuwepo katika Umma? Walikuwa walevi, wazinifu, wezi au
majambazi? Hii haikuwa sababu kama inavyoonekana kwenye kumbukumbu za
kihistoria kama ushahidi, wakati Kiongozi wa Mashahidi (a.s) alipoondoka
Makka Umma haukuwa unajishughulisha na ulevi na pombe, walikuwa
wakijishughulisha na ibada za Hijjah; halikadhalika wakati alipoondoka
Madina Umma haukuwa umejitumbukiza katika unywaji wa pombe, bali
walikuwa wamejishughulisha na Ziara ya kaburi la Mtukufu Mtume
(s.a.w.w). "Ewe Aba Abdillah (Hussein)! Unasema kwamba unatoka kwa ajili
ya kuutengeneza Umma, lakini Umma huu uko katika kushughulika na
Hijjah, Ziara ya kaburi la Mtume na ibada mbalimbali, hivyo ni
matengenezo (mageuzi) ya aina gani unayopanga kwa ajili Umma huu ambao
unaonekana kuwa na mageuzi tayari? Yeye anasema ufisadi mmoja mkubwa
umeibuka katika jamii hii. Ni ufisadi gani huo? Mtu kama Yazid amechukua
madaraka, amekaa juu ya vichwa vyao, amenyakua madaraka ya utawala na
kisha ametangaza Halali kama Haramu na Haramu kama Halali, amevuka
mipaka ya Uislam na pamoja na yote haya yanayotokea mbele ya Umma bado
hautambuhi. Maradhi ambayo Umma huu umeyapata ni yale ya kupumbaa na
kutokujali. Niliwaambia kuvua Ihram zao (mavazi ya HIjjah), lakini
walikuwa wana hamasa zaidi kuhusu ibada (hiyo ya Hijjah) kiasi kwamba
walimuacha Imam wa Umma akiwa ametengwa kwa ajili ya ibada. Walikuwa na
mipango ya kukaa Mina, Arafa ili kupata malipo (Thawaab), kisha wachinje
wanyama wao huko Mina na kwa dhabihu hizo wafanye shughuli za ustawi wa
jamii. Hata leo Umma una hamu ya juu sana ya kufanya shughuli za ustawi
wa kijamii kama ilivyokuwa zama hizo, na kama kwa matokeo ya hamasa yao
kuhusu ibada (zisizo za kiroho) na ustawi wa kijamii wanakuwa wazembe,
wasio na hisia na kutokujali kuhusu mtu kama Yazid kuwa Kiongozi wao.
Hivyo ufisadi wa Umma hauna maana kwao na kutokuwa huku na maana ni kifo
cha Umma na jamii._ "Ewe Aba Abdillah! Hivyo vipi utauamsha Umma huu?
Yeye (a.s) alisema: "Nimekusudia kufanya kuamrisha mema na kukataza
maovu." Hii ni kwa sababu kinachosababisha kifo cha jamii ni kuacha
kufanya kuamrisha mema na kukataza maovu. Nataka kuihuisha jamii hii
iliyokufa kwa kufanya matendo haya. Kuamrisha mema ni nini? Haina maana
ya kuvaa Suluali fupi, kufuga ndevu au kukaa kwa adabu, kufanya matendo
fulani ukielekea Mashariki au Magharibi au kuhoji watu kuhusu mtindo wao
wa kuongea. Kuamrisha mema ni kuufanya Umma usiojali wawe wenye kujali
kuhusu mambo ya jamii; ni kujenga hisia katika Umma usio na hisia. Ni
kuwaleta watazamaji kutoka nje ya uwanja wa michezo na kuwaingiza kwenye
uwanja. Uovu mkubwa ni kuwa wapumbavu wasio na hisia, na hili
lilitangazwa na kiongozi wa Mashahidi (a.s) kama uovu mkubwa, wakati
ambapo alisema: "Je, hamuoni kwamba haki haitekelezwi, hamuoni kwamba
batili haikatazwi?" Rejea: (Musawate Kalemate Imam Hussain (a.s) - Uk.
356). Imam (a.s) alikuwa anawaambia kwamba mmekuwa vipofu; hamuwezi
kuona kwamba haki inavunjwa na ninyi mmekaa kama watazamaji walio kimya.
Huu ulikuwa uovu mkubwa kwamba watu wamekuwa wazembe, bila hisia na
watazamaji wakimya kwenye udhalimu. Ukosefu huu wa hisia unaweza kufikia
kiasi kwamba mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) anauliwa Kishahidi pale Karbala
na watu hawa walikuwa wanaangalia kama watazamaji wakiwa wamekaa mjini
kufa. Na wale mateka ambao waliachwa nyuma kule Karbala, wakati
walipowasili Kufa watazamaji walionesha tu huzuni zao kwa kuomboleza.
Bint wa Zahra (a.s) alitoa hotuba akieleza kwamba ninyi ni wahaini,
wasaliti na watazamaji ambao wamekaa kwenye uwanja wa michezo na
kuonesha huzuni kwa mateka na kuomboleza juu ya Mashahidi wa Karbala.
Haki gani wanayo watazamaji kama ninyi ya kuomboleza juu ya watu wa
Karbala? Dhuria wa Mtume (a.s) wanauliwa na kuwa wafungwa, na watazamaji
hawa wakimya walikuwa wanaangalia tu wakiishia kwenye kuomboleza. Na
Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi