IMAM KHOMEIN (R.A) MFANO BORA WA MTU HURU:-

Leo Ummah wote wa Waislam ambao hujifikiria wenyewe kama safi na wengine (Makafiri) kama wachafu; Serikali za Waislam, wote wanakula "Lumazat" (Mabaki ya chakula) za wengine.

Israel imefunua mdomo wake na watu hawa wanachukua vijiti vya meno na kuanza kula vipande vya nyama kutoka kwenye meno machafu ya Israel. Marekani imeonesha meno yake na watu wengi wa Serikali za Waislam wakaanza kufaidi mabaki ya chakula kutoka kwenye meno yake. Kama huu sio ufungwa, utumwa na udhalili, basi ni nini? Hii ndio inaitwa Ukombozi na uhuru ambapo mnaondoa mabaki ya chakula kutoka kwenye meno ya hawa wanaojiita taifa kubwa na kisha kujaza tumbo la Ummah wenu kwayo?

Viongozi wetu na Mawaziri wanasema kwamba tuna ufinyu wa bajeti, tuna madeni na kwa hiyo tumefanywa wafungwa katika mikono ya wengine. Tumekuwa wafungwa wa Benk ya dunia na mashirika mengine ya fedha. Sio kwamba wametununua au tumeuzwa kwao, walikuwa wanafurahia chakula chao wenyewe, lakini basi baadhi ya mabaki ya chakula yalibakia kwenye meno yao. Baadhi ya viongozi wetu mashuhuri ambao walikuwa wenye kuutakia mema Ummah, ambao kwa ajili ya ustawi wa nchi, walikwenda kwao na kuwaomba wafunue midomo yao ili kwamba waweze kuondoa mabaki ya chakula na kuyaweka kwenye matumbo ya watu wao.

Kama tukimuuliza Ali (a.s) kuhusu hali ya Waislam, Je, tuko huru na wema? Je, hali hii yaweza kuchukuliwa kama hali ya Ukombozi na uhuru? Ali (a.s) atatupa jibu hili hili: "Ni nani mtu yule huru anaye hiari kuacha "Lumazat" (Mabaki ya chakula) kwa thamani yaliyonayo?"

IMAM KHOMEIN (R.A) alisikia tanafasi na maombi ya Ali (a.s) na kwa maneno ya kimatendo alisema kwamba mimi ni mtu huru, mimi ni yule mtu huru ambaye si tu atazika hii "Lumazat" (mabaki ya chakula) kwenye meno yenyewe, bali badala yake nitayavunja na meno yenyewe pia, ili mataifa mengine ya Waislam yaondokane na kula haya mabaki ya chakula.

Ufalme wa Iran ulikwa na kila kitu cha kula lakini Mfalme wake amekuwa na tabia ya kula mabaki haya ya chakula, alizoea kuondoa "Lumazat" kutoka midomo ya wengine na kuiweka kwenye midomo ya Waislam. Mtoto wa Ali (a.s) aliingia kwenye uwanja wa mapambano na kwa kuizika "Lumazat" (mabaki ya chakula) kwenye meno pia aliyavunja meno. Hili lilikuwa somo la uhuru ambalo Imam Khomein (r.a) alilichukua kutoka kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s). Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi