Misimamo ya viongozi wa Uingereza dhidi ya wananchi wa Bahrain na
uungaji mkono wao kwa utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa, vimekabiliwa
na radiamali za wananchi na taasisi za kiraia za nchini humo. Kuhusiana
na suala hilo, wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa katika
maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kulaani msimamo wa kiburi
na wa uingiliaji wa Ian Lindsay, Balozi wa Uingereza huko Bahrain
katika kuunga mkono utawala wa kidikteta wa Aal Khalifa. Waandamanaji
walibeba mabango na maberamu yenye maandishi yanayompinga balozi wa
Uingereza nchini Bahrain. Aidha wamelaani matamshi ya uingiliaji ya
Balozi wa Uingereza nchini humo na kuitaka serikali ya London
kumbadilisha balozi wake huyo huko Manama sambamba na serikali hiyo
kubadili siasa zake katika kuunga mkono utawala wa kifalme wa Aal
Khalifa. Wananchi wa Bahrain pia walikuwa wakitoa nara na shaari za
kupinga kujengwa vituo vya kijeshi vya Uingereza nchini mwao na
kusisitiza kuwa wataendeleza maandamano yao ya amani hadi matakwa yao
yatakapopatiwa ufumbuzi. Vikosi vya usalama vya utawala wa Bahrain pia
kama kawaida vilitumia gesi ya kutoa machozi kukandamiza na kuzima
maandamano hayo ya amani ya wananchi, hatua iliyopelekea watu kadhaa
kujeruhiwa na kutiwa nguvuni. Balozi wa Uingereza nchini Bahrain hivi
karibuni alitoa matamshi ya uingiliaji masuala ya nchi hiyo akikosoa
kususiwa na wananchi uchaguzi wa kimaonyesho wa bunge la utawala wa Aal
Khalifa. Pande mbili za Uingereza na Bahrain, juzi zilisaini makubaliano
ya kujenga kituo cha jeshi la majini la Uingereza huko Bahrain katika
fremu ya uuungaji mkono wa London kwa utawala wa kidikteta wa Aal
Khalifa. Gazeti la Independent linalochapishwa mjini London liliandika
kuwa, Bahrain ndiyo itakayotoa pesa nyingi zaidi kwa ajili ya ujenzi wa
kituo hicho cha kijeshi. Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilitangaza
kufikiwa makubaliano kati ya nchi mbili hizo kwa ajili ya kuimarisha
uwepo wa vikosi vya majini vya Uingereza katika bandari ya Salman nchini
Bahrain, ambayo ni makazi ya kudumu ya manowari nne za Uingereza. Hii
ni katika hali ambayo Muungano wa Februari 14 wa Bahrain umeituhumu
serikali ya Uingereza kuwa inashirikiana na utawala wa Aal Khalifa
katika kumwaga damu za wananchi wa Bahrain. Muungano huo jana ulitoa
taarifa na kuyataja makubaliano ya kijeshi yaliyosainiwa na serikali za
Uingereza na Bahrain kwa minajili ya kujenga kituo cha jeshi la majini
la Uingereza nchini Bahrain kuwa ni "makubaliano meusi" na kueleza kuwa
makubaliano hayo yanaonyesha namna utawala wa Aal Khalifa
unavyowategemea pakubwa maghasibu na wakoloni. Muungano wa Februari 14
wa Bahrain umesema kuwa, Hamad bin Issa Aal Khalifa, Mfalme wa Bahrain
yuko tayari kufanya lolote lile ili tu asalie katika uongozi wake
unaolegalega. Taasisi hiyo ya Bahrain imesema kuwa inapinga makubaliano
yote ya kijeshi yaliyosainiwa na utawala wa Aal Khalifa na kwamba
inapinga pia matamshi ya Ian Lindsay, Balozi wa Uingereza mjini Manama
yanayodhihirisha chuki za wazi za serikali ya London kwa wananchi wa
Bahrain. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/ uchambuzi/item/ 45029-upinzani-mkali-wa-wan anchi-wa-bahrain-kwa-siasa -za-uingereza
UHUSIANO WA ISRAEL NA MAGAIDI WA KITAKFIRI SYRIA.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepokea ripoti inayothibitisha kuwepo uhusiano wa karibu kati ya magaidi wa Kitakfiri nchini Syria na utawala haramu wa Israel. Ripoti hiyo imetolewa na Kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Uangalizi wa Uwekaji Chini Silaha, UNDOF ambacho tokea mwaka 1974 kimekuwa katika Miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel. Katika ripoti yake, kikosi cha UNDOF kimesema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maafisa wa Israel na magaidi wa kitakfiri wanaopata himaya ya kigeni nchini Syria. Ripoti hiyo imesema uhusiano huo umekuwepo katika kipindi cha miezi 18 iliyopita. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeendelea kudokeza kuwa Israel imekuwa ikiwapatia matibabu magaidi wa Kitakfiri waliojieruhiwa Syria na kwamba wamekuwa wakitibiwa katika hospitali za Kizayuni za Safed na Nahariya. Maafisa hao wa Umoja wa Mataifa wamesema wameshuhudia wanajeshi wa Israel wakiwapa silaha magaidi wa kitakfiri wanaopigana dhidi ya serikali halali ya Rais Bashar al Assad wa Syria. Hivi karibuni pia Alexander Prokhanov mshauri mwandamizi wa Rais Vladimir Putin wa Russia alifichua kuwa Shirika la Kijasusi la Israel, Mossad, limechukua jukumu la kutoa mafunzo ya kijasusi kwa vinara wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL).
Alexander Prokhanov pia amedokeza kuwa maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi kutoka Israel wamekuwa wakishiriki katika oparesheni za kigaidi za kundi la Daesh katika eneo la Mashariki ya Kati. Kadiri muda unavyosonga mbele, inazidi kubainika kuwa kweli kauli ya viongozi wa Syria ambao wamekuwa wakisema kuwa magaidi nchini humo wanapata himaya ya nchi za Magharibi, baadhi ya nchi za eneo na utawala haramu wa Israel. Nukta ya kutaamuli hapa ni kuwa kuna ripoti kadhaa ambazo zimefichua kuwepo uhusiano wa moja kwa moja kati ya magaidi hao wa Kiwahabi wa Daesh na mashirika ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Aidha baadhi ya weledi wa masuala ya kijeshi katika eneo wamefichua kuwa Abu Bakr Baghdadi, kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh, alipata mafunzo ya kijeshi huko Israel chini ya usimamizi wa majasusi wa Mossad. Halikadhalika kuna nyaraka nyingi ambazo zinaonyesha kuwa Abu Bakr Baghdadi amekuwa na uhusiano wa karibu na wa mara kwa mara na mashirika ya kijasusi ya Marekani. Uhusiano huo ni jambo linalobainisha wazi utambulisho halisi wa Daesh na makundi mengine ya kigaidi, Kitakfiri na Kiwahabi. Hayo ni makundi ambayo yameundwa kwa msaada wa moja kwa moja wa kifedha kutoka Marekani na Saudi Arabia na hivi sasa yanaendeleza ugaidi na fitina zao chini ya himaya na uongozi wa Israel na madola ya Magharibi. Makundi hayo ya Kitakfiri yanatekeleza kila aina ya jinai na unyama sawa na ule wa Wazayuni ili kufikia malengo yao haramu. Hakuna shaka kuwa utawala bandia wa Israel unatoa fursa iliyojitokeza kueneza sera zake za kujitanua dhidi ya Syria ili kuiondoa nchi hiyo ya Kiarabu katika duara la mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni katika eneo. Ikumbukwe kuwa Syria imekuwa mstari wa mbele katika kupigania ukombozi wa Wapalestina ambao ardhi zao zimekaliwa kwa mabavu na Israel. Ni katika fremu ya njama za kuondoa Syria katika dura hilo ndio machafuko yakaibuliwa nchini humo tokea mwaka 2011. Ni wazi kuwa utawala haramu wa Israel unayapatia himaya makundi ya kigaidi na kitakfiri yanayopigana dhidi ya serikali halali ya Syria ili kuishughulisha nchi hiyo na mapigano ya ndani. Hakuna shaka kuwa Syria inakabiliwa na njama hatari sana inayotekelezwa na utawala bandia wa Israel, madola ya nchi za magharibi hasa Marekani pamoja na waitifaki wao katika eneo ambao wanayapa himaya makundi ya Kiwahabi na Kitakfiri yanayotekeleza hujuma za kigaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu.