Kama tukitafakari juu ya kauli za Imam Hussein (a.s) wakati wa safari
yake kutoka katika ardhi ya Madina kwenda katika ardhi ya Karbala,
tunaona wazi katika sehemu nyingi za kauli zake zinahusiana na Heshima,
na upatikanaji wa Hadhi. Karbala inatufunza somo juu ya upatikanaji wa
Heshima na Hadhi na utukufu wa Mwanadamu. Katika jamii kuishi na
wakandamizaji, kupitisha hata siku moja ya maisha yako chini ya ulinzi
na Utawala wao ni jambo la kidhalili kwako, Usiwe mkandamizaja katika
maisha yako wala usiwe tayari kuukubali ukandamizaji daima. Jamii ambayo
mwenendo wa maadili umepotea, wanajamii hao ni wenye hamu sana ya
heshima na hadhi ya vya duniani. Mara kadhaa huyaacha hata majukumu yao,
ibada zao na kuachilia mbali utekelezaji wake wa haki na wajibu. Kama
mtu anaambiwa kujitokeza na kutekeleza majukumu yake ya kidini na
kiutawala, jibu kwa hilo ni: "Tunaheshimiwa sana na tunayo hadhi ya hali
ya juu sana katika jamii na halikadhalika miongoni mwa jamaa zetu, watu
wanje, marafiki na maadui na tumekisimamisha cheo hiki cha heshima kwa
shida kubwa. Imenichukuwa mimi mda kufikia cheo hiki cha heshima."
Mwenyezi Mungu (s) anasema: "Na anapoambiwa: Mche Mwenyezi Mungu, hukumbuka heshima yake aliyoipata kwa kufanya dhambi." (2:206)
Hussein (a.s) aliona kwamba wengi wa wale watu wanaotukuzwa walikuwa wamekaa mjini Madina, lakini kwa ajili tu ya kulinda heshima zao, walikuwa hawanyanyui sauti zao kwenye haki. Na katika Makka pia, kwa ajili tu ya kulinda heshima zao hakuna hata mmoja wao aliyemsaidia Kiongozi wa Mashahidi (a.s). Watu maarufu walikuwepo, lakini hata hivyo hakuna aliyemsaidia Imam Hussein (a.s). Hii ni kwa sababu Ubaidullah ibn Ziad alikuwa mtu asiyekuwa na aibu na hakujali heshima na hadhi za watu hawa; hivyo, kwa ajili ya kulinda heshima na hadhi yao ya kijamii, walimuacha mtoto wa Fatma (a.s) akiwa ametengwa. Baadhi ya watu wanafurahi sana na kujifaharisha kwamba wanatukuzwa kwa hali ya juu sana kwa sababu kila mtu huwaheshimu na kuvutiwa nao katika maeneo yao. Na wengine hufanya jitihada waheshimike kwa kukiuka hata misingi mikubwa na mipaka iliyowekwa. Kama kila mtu angalikuwa anamheshimu Mtukufu Mtume (s.a.w.w), kusingekuwa na haja yoyote kwake yeye kuhama kutoka Makka. Ukweli ni kwamba watu wa Makka hawakujali heshima ya Mtume (s.a.w.w). Mtume (s.a.w.w) huyu huyu ambaye walikuwa wakimlaumu, wakimtukana, wakimtupia taka juu yake na kumpa maumivu ya aina yote hayo, alikuwa Mjumbe mpenzi mno wa Allah (s).
Je, wale waliochoma mahema ya Hussein ibn Ali (a.s) hawakujua kwamba hawa walikuwa ni watoto wa Mtume (s.a.w.w)? Kwamba hawa walikuwa ni Ahlul Bayt (Kizazi) cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w)? Kwamba walikuwa Mabinti wa Fatma (a.s) na Ali (a.s) na kwamba ilikuwa lazima wawaheshimu? Yeye Hussein (a.s) alisema kwamba nimechagua njia ya Allah na ni Allah mwenye Utukufu ambaye nimeona kwamba atanipa mimi heshima na familia yangu. Imam Hussein (a.s) amevaa heshima na kwa vazi hilo anatufundisha kama mtu anataka kuheshimiwa basi lazima atembee juu ya njia ya Hussein ibn Ali (a.s). Wale ambao walikaa ndani ya nyumba zao kwa ajili ya kuhifadhi heshima za Mabinti wao na Wake wa watoto wao, wakati walipoona Mabinti na wake wa watoto wa Imam Hussein (a.s) wakiwa kama wafungwa mjini Kufa na Damascus, walitambuwa kile kilichomaanishwa na Heshima. Ingawa watu wanaweza kukuheshimu katika maisha ya Udhalili, kazi yako itakuwa salama, nyumba yako itakuwa salama na kila kitu kitakuwa salama, lakini Udhalili sio jina la maisha.