BUSARA KATIKA DINI NI KITU CHA MUHIMU SANA

Fikra za Uislam zitaendelea kubakia hai daima kupitia wasomi na wanazuoni wa dini ya Kiislam, wasomi wa dini ya Kiislam wanatakiwa kuwa na busara kwa kuwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) anasema "Aliye na busara ni yule ambaye hajishughulishi na udanganyifu wa dunia yake kwa kuacha kutenda kwa ajili ya Akhera yake." Rejea: Ghurarul-Hikam: 1984
Uislam halisi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) utabakia hai endapo wanazuoni wa dini ya Kiislam watatumia busara na hekima katika kuyaendea mambo leo hii kumekuwa na migawanyiko katika dini ya Kiislam kwa kuwa busara imekosekana ndani ya jamii ya Kiislam.
Migawanyiko ndani ya dini ya Kiislam itatoweka endapo busara na hekima itatumika.