Sheikh Ibarahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria aliwaambia waandishi habari katika hafla hizo kwamba, mahudhurio yalikuwa makubwa mno na kwamba Imam Hussein alitaka kuleta mabadiliko katika Umma wa Kiislamu wakati huo ambapo Usilamu ulipaswa kutakaswa. Maombelezo ya Arbaini ya Imam Hussein (A.S) mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW yalifanyika pia katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan na India.
Nchini Iraq mamilioni ya wafanya ziara kutoka ndani na nje ya Iraq walikusanyika katika mji mtukufu wa Karbala na kushiriki katika mambolezo hayo muhimu. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/45160-nigeria-wahuisha-arubaini-
WAISLAM WAENDELEA KUKANDAMIZWA NCHINI AUSTRIA.
Unyanyasaji na ukandamizaji dhidi ya Waislamu bado unaendelea nchini Austria.
Kanali ya habari ya ash Shaab, leo Jumapili imelinukuu gazeti la Heute la nchini Austria likiandika kuwa, kutolewa maneno machafu hususan dhidi ya wanawake wa Kiislamu wanaovaa vazi la staha la Hijabu bado kunaendelea na kadiri siku zinavyopita ndivyo vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu vinavyoongezeka katika nchi hiyo ya Ulaya.
Gazeti la Heute limeongeza katika ripoti yake kuwa, habari za kupigwa mwanamke bikizee katika Benki ya Bawag mjini Vienna ndilo tukio la karibuni kabisa la unyanyasaji wanaofanyiwa Waislamu nchini Austria.
Gazeti hilo limeongeza kuwa, mwanamme mmoja aliingia katika benki hiyo na kumpiga teke mwanamke huyo Muislamu mwenye umri wa miaka 60 na kumvunja tindi kadhaa za mgongo. Gazeti hilo limeongeza kuwa, mhalifu aliyempiga bikizee huyo Muislamu ametiwa mbaroni na ameshafunguliwa mashtaka mahakamani.
Ripoti zinaonesha kuwa, udhalilishaji na unyanyasaji dhidi ya Waislamu unafanyika pia kwa kupaka uchafu katika kuta za misikiti, kuning'iniza vichwa vya nguruwe katika shule za Waislamu zinazoendelea kujengwa na kubadilisha kikhabithi majina ya mitaa ya maeneo yenye Waislamu wengi nchini Austria.