Kwa mara nyingine tena Umoja wa Mataifa umeonya juu ya jinai dhidi ya Waislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Philip Luke afisa wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR katika masuala ya kiraia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, alisema jana kuwa, hali ya Waislamu wa nchi hiyo inakumbusha ukatili wa kutisha uliowahi kutokea huko Srebrenica wakati wa vita vya Bosnia katika muongo wa 1990. Philip ameongeza kuwa, mwenendo wa mauaji ya umati dhidi ya Waislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati bado unaendelea kila siku. Afisa huyo wa UNHCR katika masuala ya kiraia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti kabla ya kushuhudiwa mauaji ya umati kama yale yaliyotokea mjini Srebrenica mashariki mwa Bosnia. Ni vyema kukumbusha kuwa, katika mauaji ya umati huko Srebrenica karibu wakazi elfu nane wa mji huo waliuliwa na vikosi vya jeshi la Serbia, nchi ambayo zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wake ni Wakristo. Mauaji hayo yanatajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kutokea barani Ulaya, baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Aidha mauaji hayo yalijiri huku karibu askari 400 wa kulinda amani wenye silaha, wakiwa katika eneo la tukio bila kuchukua hatua zozote za kuzuia mauaji hayo ya umati yaliyofanywa na Wakristo wa Serbia dhidi ya Waislamu wa Bosnia.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amekosoa vikali kimya cha
jamii ya kimataifa mbele ya mauaji ya umati yanayofanyika katika Jamhuri
ya Afrika ya Kati dhidi ya Waislamu. Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami
amebainisha masikitiko yake kuwa makundi ya Wakristo wenye misimamo
mikali wameachwa kuendelea na mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu katika
nchi hiyo ya Kiafrika. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ametoa mfano wa
namna Waislamu 70 wakiwemo wanawake na watoto walivyouawa katika kijiji
kimoja huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Amesema kama ambavyo taasisi za
kimataifa zimeonya, iwapo hatua hazitachukuliwa, basi hakutabakia
Mwislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ayatullah Khatami amesema
mauaji ya Waislamu katika nchi hiyo ya Kiafrika ni sehemu ya wimbi la
chuki dhidi ya Uislamu duniani, chuki ambazo amesema zinaenezwa na
madola ya kibeberu na kiistikbari. Ameongeza kuwa chuki hizo zinatokana
na kuibuka wimbi kubwa la kuenea Uislamu duniani. Ayatullah Khatami
ameongeza kuwa, Uislamu halisi wa Mtume Muhammad SAW ni nguvu kubwa
mbele ya madola ya kibeberu na utawala wa Kizayuni. Aidha amesema kuwa
hivi sasa Iran ni makao ya Uislamu huo halisi na hii ndio sababu maadui
wanaiogopa Iran.
Ayatullah Khatami ameendelea kusema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndiye adui anayechukiwa zaidi na Waislamu. Ayatullah Khatami amesema Marekani inataka Uislamu wa Kimarekani ambao unafuatwa na watawala wa nchi za Kiarabu kwani ni kwa maslahi ya malengo yake haramu. Aidha amekosoa vikali Marekani na Saudi Arabia kwa kuwatumia silaha magaidi nchini Syria na kusema kwa hatua yao hiyo, wanachochea mauaji ya Waislamu wa Syria.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa pia ameulaani vikali utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain kwa kuendelea kuwaua Waislamu wanaoandamana kwa amani nchini humo.
Kwingineko katika hotuba yake Ayatullah Khatami amesema vikwazo vyote vya upande mmoja vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran vitasambratatishwa kupitia 'uchumi wa kusimama kidete'. Ayatullah Khatami ameongeza kuwa, uchumi wa kusimama kidete ni hatua kuelekea katika uhuru kamili wa kiuchumi nchini Iran na hivyo kuondoa kabisa utegemezi wa kigeni. Ameendelea kusema kuwa uchumi wa kusimama kidete unategemea ujuzi, elimu na teknolojia ya ndani ya nchi na uadilifu. Ameendelea kusema kuwa kwa kutegemea mamilioni ya wataalamu Wairani, miundo msingi iliyopo na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi, Iran inaweza kufanikiwa katika sera ya 'uchumi wa kusimama kidete'.