JIHAD ISLAMU: MAREKANI INATAKA KUIMALIZA PALESTINA:


Viongozi wa ngazi za juu wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina wamesema kuwa Marekani inafanya njama za kuangamiza kabisa suala la Palestina.

Khalid al Batsh ambaye ni miongoni mwa viongozi waandamazi wa harakati ya Jihad Islami amesema serikali ya Marekani kupitia juhudi zinazofanywa na Waziri wake wa Mambo ya Nje John Kerry, inafanya njama za kupoteza kabisa haki za taifa la Palestina. Ameitaka serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuondoka katika mazungumzo ya suluhu na utawala ghasibu wa Israel na kusema baadhi ya nchi za Kiarabu zinaunga mkono malengo ya utawala haramu wa Israel.

Wakati huo huo Muhamamd al Hindi ambaye pia ni kiongozi mwandamizi wa Juhad Islami amesema serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina inayoongozwa na Mahmud Abbas imelegeza kamba kuhusu masuala ya wakimbizi wa Kipalestina waliofukuzwa katika nchi yao na kadhia ya Quds Tukufu katika mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani kati ya utawala haramu na Mamlaka ya Ndani. (irib)