Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani. Akizungumza leo mbele ya hadhara kubwa ya wananchi wa matabaka mbalimbali kutoka mkoa wa Qum kwa mnasaba wa maadhimisho ya kutimia miaka 36 tokea ilipojiri harakati kubwa ya kihistoria ya wananchi wa Qum tarehe 9 Januari 1978, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ameelezea matamshi ya chuki yanayotolewa na shakhsia, duru za kisiasa na vyombo vya habari vya Marekani yaliyo dhidi ya mfumo wa Kiislamu na wananchi wa Iran, yakiwemo madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini na kuongeza kuwa, kila mtu anazungumzia suala la haki za binadamu, lakini Wamarekani hawana haki hata kidogo ya kuzungumzia suala hilo, kwani serikali yao ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani. Akielezea uungaji mkono unaofanywa na Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel katika jinai zinazotendwa na utawala huo dhidi ya wananchi wa Palestina wakiwemo wakaazi wa eneo la Ukanda wa Gaza na hata kuwazuia wananchi hao wasipate huduma za chakula na madawa, Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, vitendo vyote hivyo vinaonyesha wazi ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala huo ghasibu ukishirikiana na serikali ya Washington. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, Marekani na nchi nyingi za Magharibi zinapaswa kutoa majibu kwa fikra za walio wengi duniani, kuhusiana na vitendo vya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na nchi hizo. Akizungumzia mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea kati ya Iran na kundi la mataifa sita yenye nguvu duniani, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, mazungumzo ya Iran na nchi za Magharibi hayakutokana na uwekwaji vikwazo, bali Jamhuri ya Kiislamu itaingia kwenye mazungumzo yoyote kwa mujibu wa misimamo yake. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, hata kwenye mazungumzo ya hivi karibuni Marekani imeonyesha wazi uadui wake ilionao dhidi ya Iran na Uislamu, na nchi hiyo imeonyesha wazi kushindwa kukabiliana na taifa la Iran. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza ulazima wa kuzingatiwa masuala yaliyopita na kupata ibra katika nukta hasi na chanya na kusisitiza kuwa, mtu asijisahau na kudhani kwamba leo hii maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu wameacha uadui wao, kwani adui anaweza kutumia stratijia ya kulegeza msimamo, hivyo nasi hatupaswi kuhadaika na tabasamu la adui. (irib)
MAREKANI, MKIUKAJI MKUBWA WA HAKI ZA BINADAMU: