Waovu miongoni mwa Wayahudi walikutana toka sehemu mbalimbali za Ulimwengu ili wapole ardhi isiyokuwa yao na wakawafukuza watu wake kwa nguvu na mabavu kisha wakajenga dola ya Kidhalimu wakaiita Israili na walitumia kila mbinu na hila kuwavuta walio mfanoa wao kutoka nchi mbalimbali, na na karibu idadi yao imefikia Milioni 5, wanaishi katika jamii kubwa ya Kiarabu ya Kiislam inayokaribia bilioni moja na robo ya wananchi, na wote wanawatazama Wayahudi waliovamia na wanyang'anyi waliyopora, kwa mtazamo wa kupinga na uadui, na katika ardhi ya Palestina waliyoiteka na kuipola hakuna utajiri wa kiasili wenye kuonekana.
Lakini hawa Wayahudi pamoja na upya wao na dola yao changa ambayo muda wake hauzidi historia yake ya nusu karne, na licha ya kwamba wao ni mchanganyiko usioafikiana, na kwamba mazingira yanayowazunguka ni ya hofu na yasiyo na utulivu, lakini wao wameweza kujenga katika dola yao nguvu inayoogopesha nchi za eneo hilo, inakwenda mbio kulitawala eneo hilo na wamepata mafanikio makubwa na mabadiliko ya kielimu, kiviwanda na uzalishaji unaoshangaza.
Ni sahihi kwamba wao wanapata msaada toka Mashariki na Magharibi na hususani kutoka Marekani, lakini kwa usahihi msaada huu haukuja kwa ajili ya neema ya macho ya Wayahudi bali ni kwa kuwa wao walilazimisha nafsi zao kwa juhudi zao na kujituma kwao, na anayesoma nafasi ya kikundi cha Kiyahudi huko Marekani na Urusi anafahamu ukweli huu, kama ambavyo wao kwa juhudi zao waliweza kuuelewa msaada huu na wakaufasiri kwa kujenga nguvu na wakafaulu kwa kiasi kikubwa iwezekanavyo katika kuimalisha uwepo wao wa Kiuadui.
Waliiba na kunyang'anya ardhi ndogo lakini ni sehemu Tukufu na ghali kati ya ardhi kubwa na pana sana za Kiislam, kisha wamejenga jengo lenye nguvu lenye kuendelea kielimu, kiharakati na kujituma, wakati ardhi nyingi za Kiislam na nchi zao wanakabiliwa na hali ya kutokuendelea na udhaifu wa kurudi nyuma. Vipi wanyang'anyi na wavamizi wanaweza kufanya harakati na kujituma katika ardhi isiyokuwa yao? Na ni vipi Waislam wamedumaa katika nchi zao?
Moja ya takwimu inayotia uchungu inasema: "Hakika pato la Israil yenye ubaguzi lilifikia dola Milioni 78.1 mwaka 1994 na idadi ya wakazi wake ni Milioni 5.4, wakati idadi ya wakazi wa Misri, Syria, Jordan na Palestina inafikia Milioni 83.3 lakini pato lao wote ni chache kuliko pato la Israili."
Hapo kabla kwa miongo mingi Israili ilikuwa inahesabiwa ni moja ya nchi zenye kusaidiwa, yenye kupata msaada wa kimali toka asasi za Kimataifa, lakini tangu mwaka 1976 yaani baada ya miaka 28 takribani tangu kuasisiwa kwake, inahesabiwa kuwa ni nchi iliyoendelea isiyostahiki mikopo ya Benki ya Dunia.
Na wastani wa uzalishaji wa jumla wa kila Mwisrail mwaka 1995 umefikia hadi dola za Kiamerika 16,000 nayo ni idadi inayoikaribia Uingereza ambayo inafikia dola 18,700.
Na katika mwaka 1997 kulingana na maelezo ya Waziri wa fedha wa Israili, uzalishaji wa jumla wa kila mtu kwa mwaka umefikia dola 17,000.
Na baada ya muda wa kukua kukubwa ndani ya muda wa kati ya mwaka 1990-1996 ongezeko la uzalishaji limefikia asilimia 6 kwa sababu ya kujipanua katika nyanja zenye kukua ikiwemo sekta ya ufundi na elektoroniki.
Na kuna zaidi ya Mashirika mia moja ya Kiisrail yamesambaa Burswah (Nasdaka) New York huko Marekani, mashuhuri kwa mashirika ya kiufundi ya hali ya juu, jambo linaloifanya kuwa dola ya kwanza katika idadi ya mashirika yaliyosambaa Marekani. Rejea: As-Sharq al-Ausat: Jaridatu Yaumiyatu la London la tarehe 10/07/1999 Uk.14