Mgogoro wa Syria umeingia kwenye hatua ya
hatari sana kutokana na kuendelea vitendo vya Marekani na nchi kadhaa za
eneo la Mashariki ya Kati vya kuingilia kati na kuuchochea mgogoro wa
Syria, na hasa baada ya Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia kutoa matamshi yasiyo ya kimantiki kwa
kudai kwamba, Iran ndiyo nchi inayopasa kulaumiwa kuhusu mgogoro wa
Syria.
Hivi karibuni, Saud al Feisal, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Saudi Arabia akizungumza na John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alidai kuwa, harakati za Iran na Hizbullah ya Lebanon nchini Syria ni "hatari sana." Sayyid Abbas Araqchi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, matamshi ya Saud al Feisal yamejaa migongano. Sayyid Araqchi amesema kuwa, madai yanayokaririwa mara kwa mara ya kuingiliaji Iran mgogoro wa Syria yanatolewa katika hali ambayo, Saudi Arabia mbali na kuingilia kijeshi mgogoro wa Bahrain na kukiuka waziwazi sheria na makubaliano ya kimataifa, imekuwa ikiwapatia magaidi wa Syria silaha nyepesi na nzito, na hivyo kushiriki moja kwa moja kwenye jinai zinazofanywa na magaidi hao nchini Syria dhidi ya wananchi wasio na hatia wa nchi hiyo.
Madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia dhidi ya Iran yanatolewa katika hali ambayo, kwenye mazungumzo yake na John Kerry alisema bila kificho kuwa, serikali ya Riyadh itaendelea kuwaunga mkono kisilaha na kifedha magaidi wa Syria.
Hapana shaka kuwa, mgogoro wa Syria umekuwa tata zaidi kutokana na baadhi ya nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na Uingereza pamoja na nchi za eneo kama vile Saudi Arabia, Uturuki na Qatar kuwapelekea silaha magaidi wa Syria na kusababisha mgogoro wa nchi hiyo kuwa mkubwa na tata zaidi. Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uturuki, Saudi Arabia na Qatar tokea awali hazikuzingatia kabisa mapendekezo yaliyotolewa na nchi nyingine ya kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za mazungumzo; na badala yake zilielekeza nguvu zao za kifedha na kisilaha kwa kuyasaidia kwa kila namna makundi ya kigaidi kwa ndoto kuwa zingeliweza kuuangusha utawala wa Rais Bashar al Assad aliyechaguliwa na wananchi wa nchi hiyo. Nchi hizo hazikuzingatia hata kidogo matakwa na irada za wananchi wa Syria na hivyo kusababisha kuwa tata zaidi mgogoro wa nchi hiyo, na hata zimefikia hadi ya kuyapatia makundi ya waasi nchini humo nguvu ya kiutendaji, bila ya ridhaa ya wananchi wa Syria.
Sisitizo la kuendelezwa siasa hizo zisizo za kimantiki, limepelekea nchi hiyo kutumbukia kwenye dimbwi la umwagikaji damu na mauaji ya kutisha, huku misaada inayotolewa na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu, ikizidi kuwachoche magaidi wasio na chembe za utu kuzidi kufanya jinai za kutisha dhidi ya wananchi wa dini, madhehebu na makabila yote nchini Syria.
Inaonekana ni kwa sababu hiyo ndio maana, Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia siku ya Jumatano iliyopita aliwataka viongozi wa Marekani kuweka wazi misimamo yao kuhusiana na mkutano wa kimataifa utakaojadili kadhia ya Syria uliopangwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi. Lavrov alieleza masikitiko yake ya kutokuwepo msimamo mmoja kati ya wapinzani wa serikali ya Damascus kuhusiana na kuhudhuria na mtu wa kuwawakilisha wapinzania hao kwenye mkutano huo wa Geneva 2. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesisitiza kuwa, serikali ya Syria imetangaza wazi kuwa itashiriki kwenye mkutano huo, amma wapinzani wa serikali ya Syria wana misimamo tofauti kuhusiana na kadhia hiyo.
Ni wazi kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikiunga mkono suala la kufanyika mazungumzo kati ya makundi ya wapinzani na serikali ya Syria, na kusisitiza kwamba njia ya kijeshi kamwe haitaweza kuutatua mgogoro wa nchi hiyo. Juhudi za Iran zimekuwa zikionekana kwenye kamati ya pande nne ya Misri, Iran, Saudi Arabia na Uturuki iliyobuniwa na serikali ya Cairo kwa lengo la kuutatua mgogoro wa Syria, amma Saudi Arabia na Uturuki pamoja na kwamba ni wajumbe kwenye kamati hiyo lakini zimekuwa zikikengeuka mwelekeo sahihi wa kamati hiyo wa kusaidia utatuzi wa mgogoro wa Syria.
Weledi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, Saudi Arabia ilipaswa kufanya juhudi kubwa za kutatua masuala ya ulimwengu wa Kiislamu na kutafuta njia mbadala za kuutatua kwa njia za amani mgogoro wa Syria.
Hata kama Marekani na waitifaki wake wa eneo hili zikiwemo nchi za Saudi Arabia na Qatar zina mtazamo kwamba serikali ya Syria haiwezi kupata ushindi kwenye vita ilivyobebeshwa nchi hiyo; lakini nchi hizo zinapasa kujua kwamba nchi za Magharibi na zile za kieneo, nazo pia hazitapata ushindi kwenye mgogoro wa Syria. Na hii ni katika hali ambayo, taifa la Syria lina imani kuwa hatimaye litazishinda njama zote za maadui wanaochukizwa na msimamo wa wananchi hao wa kutokubali kuburuzwa na madola ya kibeberu na kusimama kwao kidete kupambana na utawala wa Kizayuni wa Israel. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/32953-njama-za-saudi-arabia-katika-mgogoro-wa-syria