UJUMBE KWA WAPENZI WA HARAKATI ZA KIISLAM.

Bismillah Rahmanr Rahiim.
Asalaam Aleykum.

Ndugu wafuatiliaji wa harakati zetu kwa kupitia njia ya mtandao tunajua kuwa sasa mnajiuliza kwa nini picha za harakati hamzioni?, nataka mtambue kuwa kunachembechembe za wafalme zimeingia katika harakati hizi ndio maana kuna baadhi ya mambo yanakuwa magumu kwa sasa, Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an Tukufu kuwa: "Hakika Wafalme wanapouingia mji, wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili hivyo ndivyo wanavyofanya."
(Qur'an: 27:34)

Tuangalie Muawiyyah alipoandaa kumpeleka Mughira bin Shuuba kuwa gavana wake katika Mkoa wa Kuufa, mwaka wa Arobaini na moja Hijria, alimwita akamwambia:
"Kwa hakika nilitaka kukuusia mambo mengi sana, lakini nitakuachia wewe na akili yako. Na sitaacha kukuusia jambo moja, usiache kumtukana Ali na kumkashifu, na kumhurumia Uthuman na kumuombea msamaha. Na kuwatia aibu watu wa Ali na kuwatenga mbali."

Rejea:
Tarekhut Tabari: J.4 Uk. 188
Tarekh Ibn Athir: J.3 Uk. 234

Kupitia agizo hilo, Imam Ali (a.s) alilaniwa kwa muda wa miaka mingi sana. Wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) kwa jumla walishambuliwa kwa kutukanwa na kwa kuuliwa kila inapopatikana fursa hiyo. Kwa baraka za Imam Hujjah tutasimamia haki mpaka tune la mwisho.