MICHEZO NI NJIA MOJA WAPO YA KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO BAINA YA WAISLAM, BALI NA DINI ZOTE ZA MBINGUNI.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-haad Mussa, akionyesha umahiri wake katika kuchezea soka.

Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya BAKWATA Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-haad Mussa Salum (kulia) akimtoka beki wa timu pinzani ya Istiqaama ya Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Zuu, Kigamboni jijini mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.