IMAM WA UMMAH ANATAKIWA ARIDHIWE NA MWENYEZI MUNGU (S.W.T).

Bismillah Rahmanr Rahiim.

Hakuna shaka yoyote ya kuwa Ummah unamhitaji Imam, na kwamba Imam ni wajibu awe ameridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini ni nani huyo Imam alie ridhiwa na Mwenyezi Mungu?
Ikiwa Mwenyezi Mungu, baina ya elimu na ujahili, huiridhia elimu, (Sema: Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?), 1 na baina ya Usalama na maafa, anaridhia Usalama (kwa (kitabu) hicho Mwenyezi Mungu humuongoza mwenye kufuata radhi yake katika njia za Salama), 2 na baina ya hekima na upumbavu, huiridhia hekima (Humpa hekima amtakaye. Na aliyepewa hekima bila shaka amepewa Kheri nyingi), 3 na baina ya Uadilifu na Ufasiki, huridhia Uadilifu (kwa hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha Uadilifu na Hisani), 4 na baina ya Haki na Batili, Huridhia haki (Na sema: Ukweli umefika na Uongo umetoweka, hakika Uwongo ndio wenye kutoweka), 5 na baina Usawa na Kosa, anaridhia Usawa, (Hawatazungumza ila ambaye Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema amempa idhini, na atasema yaliyosawa), 6 basi yule amridhiae Mwenyezi Mungu kuwa ni Imam wa Ummah, hapana budi asifike kwa sifa zenye kuridhiwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t).

________________________
1- Suuratuz-zumar aya 9.
2- Suuratul-maaidah aya 17.
3- Suuratul-baqarah aya 269.
4- Suuratuz-nahli aya 90.
5- Suuratul-israai aya 81.
6- Suuratul-nabai aya 38.