KUMBUKUMBU YA KIFO CHA KIPENZI CHA MTUKUFU MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W), BIBI FATMA ZAHRA,.

Maulana Sheikh Hemed Jalala, 
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), akitoa Historia fupi juu ya kifo cha Bibi Fatma Zaharau, amesema Bibi Fatma Zahra aliswaliwa usiku, na waliomswalia ni Ali (a.s), Hassan, Hussein, Ammar, Mikdad, Aqil, Zubeyr, Salman, Baridah na kundi dogo la Bani Hashim. Kisha kiongozi wa Waumini Imam Ali bin Abi Talib (a.s) akaenda kumzika kwa Siri ikiwa ni kutekeleza usia wake aliopewa na Fatma Zahra,pia alimalizia kwa kuitaka Serikali ya Tanzania kuwa macho na Wakandarasi wa Majengo amesema mtu yeyote mwenye busara jambo dogo ulifanya kubwa kwa hiyo Serikali jambo la kuanguka jengo la Ghorofa kumi na sita ilifanye kubwa, hili liwesomo kwa viongozi wa manispaa, Wakandarasi na Mainjinia kwa sababu isije ikajirudi tena na Serikali iwekali kwa watu wanaousika na maswala ya ujenzi, hili tatizo lakuanguka Majengo lisije likajirudia tena na kama litajirudia tena Waziri husika ajiuzuru.
 Waumini wa Kiislam 
wakiomboleza Kifo cha Kipenzi cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), Bibi Fatima Zahra, Maombolezo hayo yalifanyika Msijid Ghadiir Khum Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Siku ya J.pili ya Tarehe 14-04-2013.
 Masheikh wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt(a.s), 
wakiongozwa na Sheikh Muhammad Abdul, msemaji mkuu wa Harakati za Ahlul-Bayt (a.s), Dar es Salaam, Tanzania, wakiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuchangia Damu Wahanga waliopatwa na ajali ya jengo la Ghorofa kumi na sita lililoanguka wiki iliyopita sehemu ya Posta karibu na Msikiti wa khoja Shia Ithna Ashariyyah, jijini Dar es Salaam.
 Sheikh Muhammad Abdul, 
Msemaji Mkuu wa Harakati za Ahlul-Bayt (a.s), akiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuchangia Damu Wagonjwa, amesema wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kumuenzi kipenzi cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa jina aitwaye Fatma Zahra (a.s) alifariki Madina siku ya tatu ya mfunguo tisa mwaka wa kumi na moja. Aliishi siku tisini na tano tangu kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Rejea: Adh-Dhuriyat-Tahirah cha Ad-Duulabiy, Uk. 151 na 199. Kashful Ghummah, Juz. 1 Uk. 503.