Bismillahir Rahmanir Rahim.
Wanazuoni wetu lazima wajitambue kuwa hapa duniani ni watumishi wa watu na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo lazima wasifike kwa sifa ya Upole ,Huruma na Heshima, unaweza kuona baadhi ya Wanazuoni wetu wanapokuwa na majina sehemu fulani basi wanajisahau kabisa kwamba wao ni watumishi wa Jamii na hujiweka mbali na jamii zilizowazunguka au hujitengenezea mazingira ya Kifalme katika sehemu zao za kazi.
Hivi kwa nini unafikiri Imam Ali bin Mussa Al-Ridha (a.s) aliitwa Ridha?
Imam wa nne anajulikana zaidi kwa jina lake la sifa (Lakabu) la Ridha kuliko jina lake halisi la Ali.
Baadhi ya watu walimuuliza Imam wetu wa tisa: "Ni kweli kama watu wanavyosema kwamba baba yako Ali bin Mussa aliitwa Ridha kwa sababu Mamun alimpa lakabu hiyo?"
Imam hakufurahi kusikia hili, alisema kwamba' "Lakabu ya Ridha alipewa baba yake na Allah Mwenyewe na sio Mamun. Allah alimpa Lakabu hii kwa sababu Allah na Mtume wake walikuwa radhi naye."
Imam wetu wa saba Hadhrat Mussa bin Ja'afar (a.s) alikuwa akisema: "Mchukulieni mtoto wangu kama Ridha na Msalimieni kama Abul Hasan kwani atawaita watu kuelekea kwenye Ridha ya Allah na Mtume wake."
Mambo makubwa katika sifa zake yaliyomfanya awe mtu bora duniani.
Alikuwa mnyenyekevu sana na aliwatendea watu wote upole, huruma na heshima bila kuangalia kama walikuwa matajiri au masikini. Zingatia tukio hili lifuatalo ambalo uonyesha unyenyekevu wa Imam Ridha (a.s):
. Ibrahim ibn Abbas Al-Suli anasema: "Sijamuona Abul Hasan Al - Ridha (a.s) akimkasirikia mtu yeyote, wala sijamuona akimuangalia mtu yeyote, wala kusikia akikataa kumfanyia mtu yeyote upendeleo iwapo hilo linawezekana. Kamwe hatanyoosha miguu yake mbele ya watu wala kuegemea katika kitu chochote wakati wale alionao hawafanyi hivyo. Kamwe hakuwaita watumishi wake na wale waliokuwa wanamsubiri kwa majina mabaya. Wakati wanapokuwa tayari kwa ajili ya kula chakula hukaa na watumishi wake na kula chakula wote pamoja nao."
Kwa kweli wakati alipokuwa safarini kwenda Marv (IRAN), mtu mmoja tajiri alikuwa anasafari naye. Wakati wa kula chakula alimuomba Imam Ridha (a.s) ale chakula naye faragha mbali na watumishi wake. Imam Ridha (a.s) akasisitiza kula chakula na watumishi wake, akihoji kwamba wote walikuwa ni watoto wa baba mmoja na mama mmoja: Adam na Hawa.
. Siku moja Imam Ridha (a.s) alikuwa na mgeni, wakati mshumaa ulipotaka kuzimika. Yule mgeni akataka kuurekebisha; Imam Ridha (a.s) akamzuiya. Imam akaurekebisha mwenyewe ule mshumaa huku akisema: "Hatutaki wageni wetu wapate shida hii."
. Siku moja wakati akiwa Marv, Imam Ridha (a.s) alikwenda kwenye hamam ya Umma (Chumba cha bafu cha Umma), kule alimkuta mtu ambaye hamjui Imam Ridha (a.s), yule mtu alimuambia Imam Ridha (a.s) amkande mwili wake. Imam Ridha (a.s) alimkanda mtu yule. Wakati watu wanaomjua Imam Ridha (a.s) walipoona tukio lile walimkasirikia sana mtu yule. Watu sasa wakaanza kuogopa na wakafikiria kwamba Imam Ridha (a.s) atamuadhibu mtu yule kwa tabia yake mbaya. Lakini Imam Ridha (a.s) akanyamaza kama vile hakuna kilichotokea.
. Siku moja mtu mmoja alimuambia Imam Ridha (a.s): "Wewe ni mbora wa watu wote." Ingawa mtu yule alisema kweli, lakini Imam Ridha (a.s) ili kuonyesha unyenyekevu alimjibu mtu yule akisema: "Usije ukaapa hivyo. Mbora kuliko mimi ni yule mtiifu zaidi kwa Allah na Mchamungu zaidi. Wallahi aya hizi za Qur'an bado zinatumika." Kisha Imam Ridha (a.s) akasoma aya zifuatazo: "....Na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane. Hakika mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na takua zaidi yenu..."
Kwa hiyo ndugu msomaji nazani umeweza kuona nijinsi gani Imam Ali bin Mussa Al-Ridha (a.s) alivyoweza kuishi na jamii yake.