MUHADHARA WA UJUE USHIA UMEFANYIKA LUSHOTO, TANGA KWA MUDA WA SIKU MBILI J.MOSI NA J.PILI.

Maulana Sheikh Hemed Jalala, 
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), kigogo post, jijini Dar es Salaam, amesema katika Muhadhara uliyofanyika Tanga wilaya ya Lushoto kuwa waislaam walikua kwenye amani toka zamani, na Madhihab zilikua zikishirikiana,Masuni na Mashia wote walikua pamoja, toka karne 16, hawakunyoosheana vidole, wala hawakusikia kwamba Maulid ni haraam. Kwa hiyo Maulana Sheikh Hemed Jalala, Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), amewanasii Waislamu wa Tanga wilaya ya Lushoto kwa kuwataka kuwa macho na Gurupu linalojiita ANSWAARU SUNNAH kuwa alina nia nzuri na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), kazi kubwa ya gurupu hili linalojiita Answaaru Sunnah ni kuvunja mambo yote ya Historia za Kiislamu na kumtumikia Mwamerika kuwagawa Waislamu duniani kote.
Waumini wa Kiislamu wakiwa katika Muhadhara wa UJUE USHIA uliyofanyika Tanga wilaya ya Lushoto.
 Mwandishi wa Mashairi ya Karbala Juma Magambilwa, akiangalia Maanzali ya Msikiti kwa ndani. MASJID KWE MLAZI, LUSHOTO, TANGA. MOB: 0658822585.