Bismillahir Rahmanir Rahim.
Mnakaribishwa katika kumbukumbu ya Tukio la Mubahala, litafanyika siku ya J.pili, ya tarehe 11-11-2012, Saa 3:00 Asubuh, Masjid Ghadiir Khum, Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Maulana Hemed Jalala atakuwa mzungumzaji wa siku hiyo. Pia kwa upande wa wanawake baada ya kumbukumbu ya tukio la Mubahala watakuwa na shughuli ya Kitchen Party.
Katibu wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), Kigogo Post, Jijini Dar es Salaam, Al-Hajj Mputa anayofuraha kuwakaribisha katika sherehe ya Harusi ya bint yake itakayofanyika tarehe 14-11-2012 siku ya J.tano Saa 10:00 Asubuh Masjid Ghadiir Khum, Kigogo Post, Jijini Dar es Salaam. Karibuni sana
TUKIO LA MUBAHALA.
Mwenyezi Mungu anasema:
"Na atakayebishana nawe katika hili baada ya ujuzi uliokujia, basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nfsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo."
(Qur'an: 3:61)
Tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi Hijria, ujumbe wa Kikristo kutoka Najirani katika nchi ya Yemen, ukiongozwa na makasisi watatu: Ahtam, Al-aaqib na Sayyid. Walikutana na Mtume (s.a.w.w) kwa majadiliano juu ya Issa (a.s) kwa kuwa Nabii Issa (a.s) alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w) akawasomea Aya:
"Hakika mfano wa Issa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia kuwa naye akawa." Wakristo wakaendelea kushikilia itikadi yao batili, ndipo Mtume (s.a.w.w) akaamrishwa na Mwenyezi Mungu katika Aya hii kuwataka wafanye maombi ili laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.
Wakristo wakawashauri viongozi wao jambo hili, akajibu: Askofu Sayyid akawaambia:
"Enyi wakristo! mimi naziona nyuso hizi (kundi la Mtume) kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, Wallahi atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki mkristo yeyote hapa duniani mpaka siku ya Kiyama."
Naye Askofu Ahtam akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza: Ewe Abulqasim! unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano haya? Mtume (s.a.w.w) akajibu Ninaapizana nanyi nikiwa na wabora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu nao ni hawa: (akawaonyesha) Ali, Fatma, Hassan, Hussein. Alipoulizwa Askofu Al'aaqib ambaye ndiye mwenyekiti wa ujumbe huo, akawaambia: "Enyi wakristo! Wallahi nyinyi mnajua kuwa Muhammad ni Nabii aliyeletwa na amekuja na ushindi ulio wazi juu ya jambo la huyu (Issa) Wallahi hakuna watu walioapizana na Nabii wakasalimika, kama mtaapizana naye mtaangamia."
Mtume (s.a.w.w) katika kupanga Kikosi chake: Mwenyezi Mungu alipoagiza: Tuwaite watoto wetu" Mtume (s.a.w.w) akamwita Hassan na Hussein. "Na wanawake wetu" Mtume (s.a.w.w) akamwita Fatma. "Na nafsi zetu" Mtume (s.a.w.w) akamwita Ali. Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: Ee Mola! Hawa ndio watu wangu.
Taz:
Tafsirul Kabir J.8 Uk. 81
Tafsirul Qurtubi J.4 Uk. 104
Tafsirul Ibn Kathir J.1 Uk. 379
Albahrul Muhiit J.3 Uk. 189
Tafsirul Khazin J.1 Uk. 359-360
Tafsirul Maraghi J.3 Uk. 175
Fat-hul Qadiir J.1 Uk. 525
Wakristo wakaogopa kuapizana na Mtume (s.a.w.w) na badala yake wakaomba sulhu kwa kutoa dirham arobaini elfu.