SHEREHE YA EID AL-GHADIIR, IMEFANYIKA KITAIFA MASJID GHADIIR KHUM, KIGOGO POST, JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA.


Maulana Hemed Jalala,
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), akiwakaribisha wageni katika Sherehe ya Eid Al-Ghadiir, iliyofanyika Kitaifa Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post, Jijini Dar es Salaam, siku ya J.pili 4-11-2012


Maulana Hemed Jalala,
Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), amesema Eid Al-Ghadiir ilikuwa siku ya mwezi 18 wa Dhulhijja 10, siku ambayo Mtume (s.a.w.w), alimtangaza Imam Ali bin Abi Talib (a.s), kuwa kiongozi wa Waislam baada ya yeye kuondoka duniani. Uislam umeifanya siku hii ni siku ya Eid kwa kuwa ndiyo siku ambayo dini ilikamilika.


 Waumini wa Kiislam  
wa Madhihabu mbalimbali wakiwa katika sherehe ya  Eid Al-Ghadiir, iliyofanyika Kitaifa Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post, Jijini Dar es Salaam.


Wakinamama 
wakisikiliza historia ya Eid Al-Ghadiir,iliyotolewa na Maulana Hemed Jalala, Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s), Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post
Jijini Dar es Salaam.


 Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran,
 akihutubia Waumini wa Kiislam katika Sherehe ya Eid Al-Ghadiir, iliyofanyika Masjid Ghadiir Khum, Kigogo post, Jijini Dar es Salaam, amesema ataendelea kudumisha ushirikiano kati ya Iran na Tanzania.