Ni mara nyingine tena imewadia siku ya Ashura mwezi kumi (10) Muharram, pia ni wakati mwingine Uislamu unapata nguvu kutokana na msukumo wa tukio la masaibu ya Karbala; na hii ni indhari na ni kumbu kumbu kwa matendo ya kishujaa yaliyofanywa na wana wa Afrika ambao waliandika ujumbe wa (haki) kweli kwa damu yao katika aridhi ya Karbala. Uislamu, pamoja na ujumbe wake kwa Ulimwengu wote, tangu hapo awali ulimpa Uhuru mwanadamu kutoka katika himaya ya Wadhalimu. Ilikuwa suala lisilozuilika kwamba kilio cha “Hapana apaseye kuabudiwa isipokuwa Allah” kingeunganisha watu wa Mataifa yote na wa Imani mbali mbali. Pamoja na ujumbe wake wa kujikomboa mwanadamu kiroho, Qur’an Tukufu imewalingania binadamu kuungana pamoja bila ya kujali rangi wala utaifa wao. “Hapana shaka mbora wenu mbele ya Allah (s.w.t) ni yule mwenye kumcha Mwenyezi Mungu” (Qur’an, 49:13).
Ni kwa aya hii mwenyezi Mungu amempa mwanadamu Haki ya Uhuru wake. Wenye kufuzu na kulipwa mema (Pepo) ni wale tu watakaotii amri zake bila kujali utaifa wao wala utukufu na ubora wa makabila yao. Kabla ya kutaja orodha ya majina ya Waafrika walijitoa Muhanga nafasi zao huko katika aridhi ya Karbala ningependa kueleza kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa damu ya Waafrika kumwagika katika maidani ya kutetea Haki. Ni ukweli usiopingika kuwa Mashahidi wa kwanza walikuwa Mwanamke Mwafrika, Sumaiyya na mumewe, Yasir. Wao walikuwa watu wa kwanza kufa Mashahidi kwa kujitoa Muhanga pale makafiri waliposhambulia Makka na kuwaua kikatili. Mtoto wao Ammar, alikuwa miongoni mwamaswahaba wa Mtume (s.a.w.w), mtu ambaye aliaminiwa sana na Mtume. Siku moja Mtume (s.a.w.w) alisema: “Ammar, utauliwa na kikundi cha makafiri. Wewe utakuwa unawaita wao kwenye Pepo (Janah) na wao watakuwa wanakuita kuingia katika moto wa Jahanamu. Ujumbe huu ulikamilika katika vita vya Siffini, wakati Ammar alipopigana bega kwa bega upanga wa Imam Ali (a.s) na kuuliwa na jeshi la Muawiyyah Khabbab bin Al-Arrat alikuwa Sahaba mwingine maarufu zama za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ambaye alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kusilimu. Naye pia alitokea katika bara la Afrika, na aliuliwa na makafiri walipoishambulia Makka wakati akipigania Haki. Huko katika ardhi ya Karbala pia, ili kuendeleza jadi ya kujitoa Muhanga, Afrika ilitoa mchango mkubwa kuutetea Uislamu. Tunapowakumbuka Mashahidi waliouliwa Karbala wapatao 72, na 12 kati yao ni kutoka katika Bara letu, kwa kweli tunafarijika kuona Afrika ilivyokuwa mstari wa mbele kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Katika siku hiyo ya msiba jeshi la maadui wa Uislamu liliwashambulia Waislamu alfajiri na mapema. Jeshi la maadui wa Uislamu lilikusudia kuwakanyaga kanyaga kwa kwato za farasi Maswahaba wote wa Imam Hussein (a.s), pamoja na familia yake na watoto wadogo. (Idadi ya Wanaume, Wanawake na watoto katika msafara wa Imam Hussein (a.s) haikuwa zaidi ya watu 100). Lakini Maswahaba watiifu wa Imam Hussein walijipanga vema na kusonga mbele. Jeshi la Muawiyyah lilikuwa na watu (Makafiri) wapatao 4,000. Mapigano makali yalianza na baada ya muda maadui walirudi nyuma.kwa Imam Hussein (a.s) haukuwa ushindi mzuri, kwa kuwa aliwapoteza miongoni mwa marafiki zake watiifu wapatao 50. Miongoni mwa Mashujaa 50 walikuwepo Waafrika saba: Salim, Zahri, Quarib bin Abdulla, Munjeh bin Salim, Saad bin al-Harth, Nasr bin Abi Naizer na Harth bin Nab-han. Majina yao hawa Mashahidi (Mashujaa) yamewekwa katika kumbu kumbu sio tu na Wanahistoria mashuhuri, bali pia na Maimamu wetu walioandika Ziyarah wakiwataja Mashahidi wote mmoja baada ya mwingine. Shaudhab, Mwafrika mwingine alikuwa Mwanazuoni maarufu wa Shariah za Kiislamu na Hadith wa wakati huo. Watu walikuwa wakisafiri msafa marefu kuja kusikiliza hekima na nasaha zake. Baada ya kusikia ukweli wa Imam Hussein (a.s) Shaudhab pamoja na rafiki yake, Abis Shakiri, waliungana na Imam Hussein (a.s) na wakafa Mashahidi katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya kuunusuru Uislamu. John; ambaye bila shaka alikuwa Mkristo aliyesilimu alikuwa Mtumwa wa Kihabeshi ambaye baada ya kufariki “Bwana” wake; alichukuliwa na familia ya Mtume ili aishi nao kama mgeni wao. Alibakia hapo kwa furaha na amani kwa muda wa miaka 30 hivi. Aliungana na Imam Hussein kwenda Karbala, ingawa alikuwa tayali ni mzee wakati huo lakini alipigana kwa nguvu zote kabla ya kuuwa. Alipoanguka chini, Imam Hussein alimwendea, na akakinyanyua kichwa chake na kukilaza juu ya paja lake na kumuombea. Hadith za Kishia zinaelezea kuwa watu wa kabila la Asad waliokuja kuwazika Mashahidi (Mashujaa) baada ya siku tatu walishangaa kuona mwili wa marehemu kung’ara na unanukia kwa manukato mazuri ya Peponi. Ulikuwa mwili wa Shujaa, John. Aquaba, pia kutoka Bara la Afrika alikuwa miongoni mwa Maswahaba waaminifu wa Imam Hussein (a.s). Imama aliacha nyaraka zake zote muhimu chini ya uangalizi wa Aquaba. Aliyeruhiwa katika vita vya Karbala, na alichukuliwa mateka pamoja na familia ya Imam. Akiwa miongoni mwa watu walioshuhudia mauaji ya Karbala, imebaki kuwa kumbu kumbu na kielelezo muhimu katika Historia. Miongoni mwa watu waliokuwa pamoja na Imam Hussein (a.s) Karbala ni Mwanamke Mwafrika, Fizza (s.a); ambaye atakumbukwa milele kutokana na Imani yake na huduma zake kwa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Nchi yake ya asili ilikuwa Nuba, ambayo hivi sasa ni Sudani. Kwanza alitoa huduma kwa Bi-Fatima bint yake Mtume. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipanga utaratibu kwamba siku moja Bi Fatima (a.s) alifanya kazi za nyumba zote na Fizza apumzike na siku ifuatayo Fizza alifanya kazi hizo na Bi Fatima (a.s) apumzike. Baada ya kufariki dunia Bi. Fatima (a.s), Fizza (s.a) aliolewa na Muislamu mcha Mungu na akaweza kuitunza familia yake, lakini uwajibikaji wake kwenye nyumba ya Imam Ali (a.s) uliendelea kama kawaida. Aliungana na Imam Hussein kwenda Karbala na kuwa pamoja nao katika madhila, maafa na masaibu yaliyowapata wanawake na watoto wa Imam katika ardhi ya Karbala. Elimu ya Qur’an ya Fizza (s.a), imeelezwa na Mwanazuoni maarufu Abul Qasiim Qushairi. Mwanazuoni huyu ameandika katika wasifu wa Fizza kwamba, kwenye miaka 20 ya mwisho wa uhai wake Fizza hakuweza kutamka neon lake mwenyewe, wakati wote alizungumza au kusoma aya kutoka katika Kitabu Kitakatifu cha Qur’an. Uislamu unajivunia watoto wa ardhi ya Afrika ambao kwa mapenzi yao walijitolea Muhanga kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w.t). Kizazi cha Imam Hussein (a.s) wakati wote walitoa heshima zao kwa Mashahidi wa Karbala maneno yafuatayo:-
“Heshima juu yenu Enyi mlioridhiwa na Allah pamoja na Waja Wake. Heshima juu yenu Enyi Wasaidizi wa Imani. Naomba Wazazi wangu wapate Heshima ya kuyaweka Maisha yao kwa ajili yenu. Mlikuwa Watakatifu na Watoharifu na mpo watakatifu na Watoharifu hapo mlipo milele. Kwa hali ya juu mmefuzu, Ninamuomba Allah aniweke pamoja nanyi ili niwe miongoni mwa wenye kufuzu”.