Swali: Je! upo uwezekano wa kuishi zaidi ya Miaka 200?

Jibu: ndio upo uwezekano wa kuishi zaidi ya miaka 200 kama maisha marefu ya hadhrat mehdi imam wetu wa zama hizi hadhrat mehdi (a.s.) alizaliwa mwaka 255 (a.s.) na yu hai hadi leo. watu hutilia shaka juu ya maisha yake marefu ya zaidi ya miaka elfu moja. ubishi upo kwamba mtu akitimiza miaka mia huwa mdhoofu, hajiwezi na pungwani, kwa hivyo vipi mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 1100 huweza kuwa na afya nzuri? suala hili hujibiwa kwa aya nyingi za qur'an, hadithi na kwa dalili za kiakili. kwanza, ni jambo dhahiri lililothibitishwa kihistoria kwamba watu wengi wakiwemo waumini na makafiri miongoni mwao, wanajulikana kuwa wameishi zaidi ya miaka elfu moja, kwa hakika tutathibitisha katika sura hii kwamba baadhi ya hao wapo hai hadi leo.
Qur'an tukufu inapozungumzia juu ya nabii yunus imeeleza: basi isingelikuwa ya kwamba yeye alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakimsabihi mwenyezi mungu vilivyo. bila shaka angelikaa tumboni mwake (samaki) mpaka siku ya baathi." (37:143 & 144). nabii yunus alikuwa binadamu. ikiwa allah kwa uwezo wake anaweza kumweka hai binadamu tumboni mwa samaki bila huyo binadamu kupata mwangaza, upepo, chakula hata maji mpaka siku ya kiyama, kwa nini haiwezekani kwake kumweka mtume wake (au mrithi wa mtume wake) hai kwa muda wa miaka 1,000 au 2,000? hakuna mtu anayeweza kutia shaka juu ya uwezo wa mungu. kwa hivyo, swali linaloweza kuulizwa ni je, ni kweli hadhrat mehdi (a.s.) yu hai, na kama yupo hai kwa nini haonekani? masuala hayo yamezungumziwa katika sura nyingine ya kitabu biki. hata masunni wamekubali na kuandika juu ya maisha marefu ya hadhrat mehdi (a.s.) hayo pia katika sura nyingine katika kitabu hiki. wafuatao ni binadamu, mitume watukufu na vile vile washirikina na makafiri ambao walijaliwa maisha marefu mno: mitume na waumini:
nabii nyh miaka 2,000 hadhrat lukman miaka 3,800 nabii suleiman miaka 700 miaka nabii hood miaka 464 nabii adam ambaye aliishi miaka 930 na kuacha ayali ya watu .40,000 nabii shish miaka 900 bibi hawa (mke wa nabii adam) miaka 930 manabii wanne ambao wangali hai hadi leo mbinguni kwa maelfu ya miaka: nabii idris alichukuliwa mbinguni wakati umri wake ulikuwa umekwishatimia miaka 890 na yupo huko kwa miaka elfu kwa maelfu. nabii issa yupo mbinguni kiasi cha miaka 2,000. makafiri na washirikina: iblis tangu milele, anak binti wa nabii adam, miaka 3,000. ouj bin anak, miaka 3,600 mfalme jamshed miaka 1,000 zahaq tazi (mpwa wa jamshed) miaka 1,000 aaad bin our bin irem saam bin nooh miaka 1,200 shaddaad, miaka 900. cyrus, mfalme wa iran miaka 1,000 dajjal, miaka 1,375 na yu hai hadi leo.

Duniani Nabii khidhr yu hai leo miaka 4,000 na hutembea dunia nzima. nabii elias yu hai kiasi cha miaka 4,000-5,000 na hutembea dunia nzima. hatimaye, hoja moja ya kirazini. ikiwa atatokea mtu mmoja akada kwamba anaweza kutembea juu ya maji, bila shaka watu wote watamzunguka na kuona kwamba kweli huyo anatembea juu ya maji na kushangazwa na kumwamini yeye kama mtu mtakatifu. lakini ikiwa baada ya rnuda mfupi atatokea mtu mwingine na kudai hilo, mshangao wa watu utapungua na hawatakuwa wengi kumwangalia mdai wa pili kama walivyomwangalia wa kwanza. dai kama hilo halitakuwa tena jambo la kushangaza. kama akitokea mdai wa tatu watu hawatashangazwa hata kidogo na hakitakuwa kitu kipya tena.
 

vile vile, ikiwa watu wengi wamekwishaishi maisha ya maelfu ya miaka ya maelfu na kwa hakika manabii khidhr na elias wamekwishaishi maisha zaidi ya miaka 4,000-5,000, na wakiwa na afya nzuri huku wakitembea dunia nzima, basi haliwezi kuwa jarnbo la kustaajabisha kuwepo hai na mwenye afya nzuri kwa imam wetu wa kumi na mbili (a.s.) kwa miaka 1,110-1,200. si ajabu wala kustaajabisha tena wakati wakristo na waislamu hukubali iblis na dajjal wapo hai hadi leo na agog magog wapo hai kwa tangu maelfu ya miaka ya zama ya alexander mkuu.
kwa hakika manabii khidhr na elias wapo hai ijapokuwa kipindi chao cha unabii na uongozi umemalizika. hiki ni kipindi cha unabii wa mtume muhammad (s.a.w.w.) na kanuni za kiislamu zilizopangwa kutokana na aya za qur'an zitadumu hadi siku ya kiyama. kwa hivyo, muda mrefu wa uhai wa manabii na mfano bora sana kuhusu maisha marefu ya imam wa zama hizi, hadhrat mehdi (a.s.) aliyejaliwa na mungu.
idadi kubwa ya wanazuoni wa kisunni wamenakili katika vitabu vyao habari juu ya kuzaliwa kwa hadhrat mehdi (a.s.) katika mwaka 255 a.h. na kuwepo hai kwake hadi leo na vile vile kunakili habari za watu walionana naye. hata hivyo, wengi wao huamini kwamba hadhrat mehdi (a.s.) hajazaliwa bado na atazaliwa katika siku za mwisho na yeye ndiye atatawala kwa insafu na usawa. sababu kuu kuhusu itikadi hii ni kwamba wakimkubali kuwa hadhrat mehdi (a.s.) amekwishazaliwa watalazimika kumkubali kama yu hai na ameghibu na bidhaa yake itakuwa kuacha imani juu ya makhalifa kumi na wawili wanaowakubali, na kufuata itikadi ya ithnaasheri ambayo inaamini kwamba ukhalifa unakomea kwa hadhrat mehdi (a.s.), imam wa kumi na mbili.
kwa wanaomkataa hadhrat mehdi (a.s.) amekwishazaliwa na yungali hai, kuwa ana pahala pake anapoishi, watoto na wahudumu wake na kukutana na watu kwa sababu tu kwamba pahala anapoishi hapakuonyeshwa katika ramani na si rahisi kufika ni kujidanganya nafsi zao. papo hapo, hao wanaomkataa imam mehdi (a.s.) wenyewe wanawaamini wale waliojificha na hawaonekani na kwamba maskani yao hayajaweza kutambulika. kwa mfano, katika kitabu cha "rehla eibne battuta" (ibne battutta aliyefariki 779 a.h.), ambacho kinaeleza juu ya safari yake ndefu kwenda arabuni, iraq, asia na china, katika juzuu la pili ukurasa 64 imenakiliwa kuwa: "katika safari yangu nilifika had! china ambako nilisimuliwa juu ya sheikh wa ajabu mwenye umri wa miaka 200, lakini hakuna mtu yeyote aliyemwona akila, kunywa wala kuzungumza na mtu mwingine. alikuwa na afya nzuri lakini hakufunga ndoa, akiishi ndani ya pango lakini akitoka nje wakati akitaka kufanya ibada. hivyo niliamua kwenda pamoja na sahibu zangu kumwona huyo sheikh pangoni mwake.tuiipofika tulimwona amesimama nje ya pango lake. nilimsalimu na akanijibu. baadaye, akaushika mkono wangu na maneno yake yalifasiriwa kwangu na mkalimani kwamba mimi ninaishi upande wa magharibi wa dunia na yeye anaishi upande wa mashariki wa dunia.
tena akaniambia kwamba katika safari yangu nimeona vitu vya kumstaajabisha na ninakumbuka kuzuru kisiwa ambamo kulikuwa hekalu moja na humo ndani nilimwona mtu ambaye alinipa sarafu kumi za dhahabu. nikamjibu kwamba tukio hilo nakumbuka vizuri sana. akanijibu kwamba mtu yule alikuwa yeye mwenyewe (sheikh). papo hapo nilimbusu mkono wake, naye akanyamaza kimya kwa muda mrefu. ghafla yeye akaingia ndani ya pango. tulimsubin nje kwa muda mrefu sana lakini hakutokea, kwa hivyo tuliamua kumfuata ndani lakini tuliambiwa kwamba hatutaweza kumwona tena. mtumishi wake alikuwa na vipande vya karatasi ambavyo alinikabidhi na humo ndani kuliandikwa kwamba sheikh amemkabidhi zawadi kwa ajili ya wageni na kwa hivyo mimi niondoke. niliposisitiza kutaka kumwona huyo sheikh mhudumu akaniambia kwamba hata nikisubiri miaka kumi sitaweza kumwona tena kwa sababu yeye haonani na mtu yeyote mara ya pili.
mimi nilihisi kuwa huyo mtu alikuwa pale pale na mimi, ila alikuwa haonekani tu. sisi tuliduwazwa na tukatoka kwenye hilo pango. mwandishi aliendelea kusema "mimi niliwasimulia tukio hakimu shaikhul islam na awahududin bukhari nao walithibitisha kwamba mtu yeyote aliyemwona huyo sheikh (huko china) mara ya kwanza hawezi kumwona tena na yule mhudumu aliyewakabidhi hiyo bahasha ni huyo mtu mwenyewe lakini alibadilisha sura yake. sahaba wake mmojawapo alithibitisha kwamba aliwahi kujificha kwa miaka 50 na kujitokeza ghafla. hakuna cho chote katika pango hilo lakini mhitaji yeyote aombapo msaada hupatiwa pesa. huyo sheikh (wa china) alisimulia hadithi ya mtume (s.a.w.w.) na kuzungumza mambo yaliyopita. yeye hudai kwamba angalikuwa wakati wa mtume mtukufu (sa.w.w.) angalimsaidia bila wasiwasi wowote. naye huwalaani vikali mno muawiya na yazid.
zaidi ya hayo katika kitabu hicho hicho juu ya safari zake mwandishi aandika kwamba awahuddin bukhari alimwambia kwamba yeye (bukhari) aliwahi kuingia ndani ya hilo pango na huyo sheik alipeana naye mkono. anakumbuka kwamba alikuwa katika kasri kubwa iliyopambwa sana na sheikh huyo alikaa juu ya kiti cha enzi na kuvaa taji kichwani mwake huku akizungukwa na magashi. aliona mito hupita na vile vile miti yenye matunda matamu. aliokota tunda moja ili ale lakini ghafla alijikuta yuko peke yake nje ya hilo pango. mandhari yale yalipotea na akajikuta peke yake. papo hapo akaondoka. mambo ya kustaajabisha kama hayo yanayomhusu sheikh yamenakiliwa katika vitabu vya sunni na huonekana kwamba waislamu wapo tayari kumwamini huyo sheikh, kuhusu kujificha kwake na miujiza ya kustaajabisha wakati hata jina lake halifahamiki. lakini, bado wanatia shaka juu ya hadhrat mehdi (a.s.), wakati qur'ani tukufu, hadithi na historia na vitabu vilivyoandikwa na waandishi wa kiislamu hutoa maelezo ya kutosheleza juu yake, kughibu kwake na miujiza yake. 


(Chanzo: http://abna.ir)