Makumi ya
maelfu ya wananchi wa Yemen wameandamana leo katika mji mkuu wa nchi
hiyo Sana'a kulaani siasa za kichokozi na kivamizi za utawala wa Aal
Saud.
Katika maandamano hayo wananchi wa Yemen mbali na kutoa sha'ar dhidi ya utawala wa Aal Saud na Marekani wamelaani mashambulio ya anga yaliyofanywa karibuni na ndege za kivita za utawala wa Aal Saud katika soko la al-Khamis mkoani Hajjah na kutaka kukomeshwa haraka mashambulio ya kinyama ya Saudia dhidi ya nchi yao.
Wananchi hao wamelaani pia kimya cha Umoja wa Mataifa na Jamii ya Kimataifa kwa jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud nchini Yemen.
Itakumbukwa kuwa watu 119 waliuawa shahidi na makumi ya wengine walijeruhiwa katika shambulio la kinyama la anga lililofanywa hivi karibuni na ndege za kivita za utawala wa Aal Saud kwenye soko la al-Khamsin mkoani Hajjah.
Hadi sasa watu wasiopungua 8,400 wameuawa na wengine zaidi ya 16,000 wamejeruhiwa tangu Saudia na washirika wake walipoanzisha mashambulio na uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wa utawala wa Aal Saud, Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi. Mashambulio hayo yameangamiza na kusababisha hasara kubwa pia kwa miundombinu ya Yemen, mbali na kulenga na kubomoa hospitali, shule, misikiti na turathi za kihistoria za nchi hiyo.../