MASJID IMAM ALI BIN ABI TALIB (A.S), TANGA WILAYA YA LUSHOTO.

Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa baadhi ya Wanaharakati huko Lushoto Mkoa wa Tanga kuwa  Msikiti ambao unajulikana kwa jina la Masjid Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ambaye ni Imam wa kwanza wa Waislam wa Madhehebu ya Shia Ithna Asharriyyah, Msikiti huo kwa sasa haupo katika hali nzuri hasa katika kipindi hiki cha mvua hivyo imelazimika kusimamisha masomo kutokana na jengo la Msikiti kupitisha maji katika baadhi ya maeneo imelazimika kukunja mabusati ya Msikiti huo huku wakisitisha shughuli zao za kila siku. Msikiti huu ndani yake kuna Madrasa ambayo inawanafunzi wasiopungua sabini (70) ambao wanajifunza Qur'an Tukufu Lugha ya Kiarabu na somo la Fiqih pia inasemekana hapo hawali kulikuwa na Shule ya Chekechea (Nursery School) ambayo ilileta muamko wa elimu kwa watoto katika kijiji hicho na kufanya vizuri katika masomo yao katika Shule za Msingi hivi sasa Shule hiyo haipo tena kutokana na kukosa watu wa kuwalipa walimu mishahara na mahitaji ya Wanafunzi sasa kumebakiwa na Madrasa nayo imekuwa mtihani kwa wana Kijiji hakuna wakuwasaidia mpaka imefikia hatua ardhi ya Msikiti huu kupewa jina la Karbala kutokana na mitihani inayowakumba katika kijiji chao kila kukicha kwao ni majonzi na masikitiko tu.