Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuzikurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, kimya cha leo cha baadhi ya tawala za Kiarabu na Kiislamu kwa jiani za kutisha za utawala wa aal-Saud huko nchini Yemen ni khiyana na usaliti kwa Uislamu na Waislamu. Ayatullah Mohsen Araki amelaani jinai za Saudi Arabia dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen na kuongeza kuwa, jinai za utawala wa Riyadh hazipaswi kunyamaziwa kimya. Ikumbukwe kuwa Saudia ilianzisha hujuma dhidi ya Yemen mnamo Machi 26 bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa. Lengo la hujuma hiyo ni kuiangusha harakati ya Ansarullah iliyoko madarakani na kumrejesha rais wa zamani wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansur Hadi ambaye ni kibaraka wa Saudia. Aghalabu ya waliopoteza maisha katika hujuma ya Saudia nchini Yemen ni raia wasio na ulinzi wakiwemo wanawake na watoto. Aidha Saudia imetumia silaha zilizopigwa marufuku kama vile mabomu ya vishada katika hujuma dhidi ya maeneo ya raia nchini Yemen.
MAAFA YA KIBINADAMU YEMEN, MTIHANI WA KIHISTORIA KWA NCHI ZINAZODAI KUTETEA HAKI ZA BINADAMU.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashambulizi ya kinyama na kikatili yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen ni makosa ya kistratijia ya serikali mwanagenzi iliyochukua madaraka hivi karibuni nchini Saudia.
Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo mapema leo katika kongamano la Mwanadamu Mwenye Huruma, Dunia Yenye Utulivu” linalofanyika kwa mnasaba wa Wiki ya Jumuiya ya Hilali Nyekundu hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa: Serikali isiyojua masuala ya kisiasa ya eneo la Mashariki ya Kati na dunia na daima imekuwa ikitatua mambo yake kwa kutumia dola za mafuta sasa inadhani kuwa inaweza kuwa na nguvu na kufikia malengo yake kwa kutumia mabomu na kuishamnbulia Yemen. Rais Rouhani ameashiria hali mbaya inayowakumba watu wa Yemen na kusema ni jukumu la kibinadamu kuwasaidia watu wa nchi hiyo iliyoathiriwa na mshambulizi ya Saudia.
Rais Rouhani amepongeza juhudi za Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran katika kuwasaidia watu wa Yemen.
Baada ya kuanza mashambulizi ya kinyama ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen, Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifanya jitihada kubwa- kama taasisi ya misaada ya kibinadamu- kujaribu kutatua matatizo ya watu walioathiriwa na vita wa Yemen, lakini serikali ya Saudia inazuia hatua hizo huku Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu likitumia sera za kibaguzi katika kuwasilisha misaada kwa waathiriwa.
Zimepita siku 45 sasa tangu nchi ya Saudi Arabia isiyojua ukweli wa mambo kuhusu jamii ya Yemen na siasa za kimataifa, ilipoanza kuishambulia nchi hiyo huku Wayemen wakiendelea kusumbuliwa na uhaba wa dawa, chakula na zana za tiba. Watu wa Yemen wanapita katika kipindi kigumu mno katika hali ambayo nchi zinazodai kushika bendera ya kutetea haki za binadamu na uhuru wa kiumbe huyo zikiangalia kwa macho tu. Mashambulizi ya sasa ya Saudia nchini Yemen na mwenendo wa jumuiya za Magharibi za kutetea haki za binadamu vimeonesha kuwa mtazamo wa kisiasa umegubika na kutawala shughuli za jumuiya hizo eti za misaada ya kibinadamu.
Mtazamo huo wa kisiasa wa jumuiya za misaada za nchi zinazodai kutetea haki za binadamu kuhusu maafa ya Yemen umekuja katika hali ambayo, nchi hizo hizo za Magharibi zimetoa suhula zao zote kwa serikali iliyo katika ndoto za mchana na mwanagenzi ya Riyadh. Kwa mfano tu gazeti la Guardian la Uingereza limeandika kuwa, kila siku karibu ndege 100 za kivita zinafanya mashambulizi nchini Yemen na kwamba 50 kati ya ndege hizo zimetengenezwa nchini Uingereza.
Kushiriki ndege na marubani wa kigeni katika mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia nchini Yemen kunazusha swali kwamba, Je, kama nchi yoyote ya Ulaya ingeshambuliwa na nchi nyingine ya kichokozi, mtazamo wa kisiasa ungegubika la kutawala masuala ya kibinadamu kama nchi za Ulaya zinavyofanya sasa kuhusiana na Yemen?
Ukweli ni kuwa kama nchi ya Ulaya ingeshambuliwa na nchi nyingine ya kichokozi basi hapana shaka kuwa, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lingetupilia mbali mtazamo wake wa sasa wa kisiasa katika masuala ya kibinadamu na kuanzisha darala la anga kwa ajili ya kuwasaidia kwa hali na mali watu wa nchi hiyo.
Kwa sasa nchi madhlumu na ya Kiislamu ya Yemen inaendelea kushambuliwa vikali kwa ndege za Saudai Arabia zinazoendeshwa na marubani wa kigeni kwa siku 45. Ndege hizo zilizotengenezwa na Wamagharibi zinakanyaga misingi yote ya ubinadamu na kulenga taasisi za kijamii na mindombinu, nyumba za raia, vituo vya afya na shule, raia wa kawaida hususan wanawake na watoto wadogo. Kwa hakika hali ya sasa ya Yemen na mauaji ya umati yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia ikiungwa mkono na washirika wake wa Kimagharibi, ni mtihani wa kihistoria kwa nchi zinazodai kushika bendera ya kutetea haki za binadamu na uhuru huku zikitazama kwa macho tu na kufarijika mbele ya mauaji ya wanawake na watoto wadogo wasio na hatia yoyote.

SAUDIA YAHUJUMU MASJID IMAM HADI AS SA'ADA.
Ndege za kivita za Saudi Arabia Jumamosi zimeendeleza hujuma zake za kikatili nchini Yemen na mara hii zimehujumu kwa mabomu msikiti wa kihistoria ujulikanao kama Masjid Imam Hadi AS katika mkoa wa Sa'ada kaskazini mwa nchi hiyo. Televisheni ya al-Masirah imeripoti kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia zimeushambulia kwa mabomu msikiti huo wa kale katika siku ya 45 ya hujuma ya kinyama dhidi ya Yemen. Raia wasiopungua 14 wamepoteza maisha katika hujuma dhidi ya msikiti huo. Halikadhalika maeneo ya Qamar na Saqayn yameshambuliwa katika mkoa huo huo. Halikadhalika hospitali ya mkoa wa Shabwah imelengwa katika hujuma ya ndege za kivita za Saudia nchini Yemen. Hujuma hizo zinajiri siku mbili baada ya wakuu wa Saudia kutangaza mpango wa usitishwaji mapigano nchini Yemen.
Ikumbukwe kuwa Saudia ilianzisha hujuma dhidi ya Yemen mnamo Machi 26 bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa. Lengo la hujuma hiyo ni kuiangusha harakati ya Ansarullah iliyoko madarakani na kumrejesha rais wa zamani wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansur Hadi ambaye ni kibaraka wa Saudia. Aghalabu ya waliopoteza maisha katika hujuma ya Saudia nchini Yemen ni raia wasio na ulinzi wakiwemo wanawake na watoto. Aidha Saudia imetumia silaha zilizopigwa marufuku kama vile mabomu ya vishada katika hujuma dhidi ya maeneo ya raia nchini Yemen.

MELI YA "UOKOZI" YA IRAN KUPELEKA MISAADA YEMEN.
Kazi ya kupakia misaada ya kibinadamu ya Shirika la Hilali Nyekundu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Meli ya Uokozi huko Bandar Abbas kusini mwa Iran imekamilika na meli hiyo yenye misaada kwa ajili ya wananchi wa Yemen iko tayari kwa ajili ya kuelekea katika nchi hiyo. Meli ya Uokozi ya Hilali Nyekundu ina tani elfu mbili mia tano za misaada ya kibinadamu ikijumuisha tani mia mbili za mchele, tani 700 za unga wa ngano, tani 400 za vyakula vya kopo, tani 50 za dawa na vifaa vya tiba, tani 50 vya maji safi ya kunywa ya chupa, mablanketi, mahema na vyombo vya jikoni. Meli hiyo ina watu 60 wakiwemo madaktari 15, waandishi habari 20, wanaharakati na shakshia wa kimataifa, walinzi watano na wafanyakazi 20 na jioni ya leo inatarajiwa kuanza safari ya kuelekea nchini Yemen kuwapelekea misaada hiyo wananchi wa nchi hiyo wanaotaabika na kuteseka kutokana na mashambulio yasiyo ya kibinadamu ya utawala wa Saudia.
RIDIAMALI YA JESHI LA YEMEN NA HARAKATI YA ANSARULLAH KUHUSU PENDEKEZO LA USITISHWAJI MAPIGANO KWA MUDA.
Wanajeshi wa Yemen pamoja na wapiganaji wa harakati ya wananchi ya Ansarullah kwa pamoja wamekaribisha pendekezo la usitishwaji mapigano kwa muda ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia raia wa kawaida wanaokabiliwa na matatizo na madhila makubwa kutokana na vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya nchi yao. Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya al-Masir, baraza la kisiasa la Ansarullah limesema linaunga mkono kusimamishwa vita kwa muda kwani uvamizi wa kidhalimu wa Saudia dhidi ya wananchi na taifa la Yemen umewasababishia wananchi wa kawaida hususan akina mama na watoto madhila na masaibu makubwa. Harakati ya wananchi ya Ansarullah imesifu juhudi zinazofanywa na nchi marafiki wa Yemen za kujaribu kuhitimisha uvamizi wa Saudi Arabia na waitifaki wake na kusisitiza kuwa mazungumzo ya kitaifa yanapaswa kuanza upya lakini kabla ya yote, Riyadh isimamishe mara moja hujuma na uvamizi wake dhidi ya Wayemen.
Pendekezo la usitishwaji vita kwa muda pia limeungwa mkono na makundi mengine yenye silaha nchini Yemen. Sharif Mahfudh, msemaji wa kundi jingine linalopigania uhuru wa wananchi wa Yemen amesema kundi lake litaheshimu makubaliano hayo ya usitishaji vita kwa muda yanayotarajiwa kuanza kutekelezwa siku ya Jumanne. Mahfudh ametaka hata meli za kibiashara ziruhusiwe kutia nanga katika bandari ya Yemen ili kurahisisha mipango ya kufikishwa misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa mashambulizi ya anga ya Saudia na waitifaki wake huko Yemen. Sharif amesisitiza kuwa, tabia ya Saudi Arabia ya kuzuia kuingizwa misaada ya kibinadamu kama vile chakula na dawa nchini Yemen ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na haki pamoja na misingi ya ubinadamu na ametaka viongozi wa Riyadh kuwajibishwa kutokana na makosa hayo.
Wizara ya Afya ya Yemen kupitia msemaji wake, Tamim al-Shami imesema iwapo kweli Saudia itaheshimu makubaliano ya usitishaji vita ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa vita basi pana haja ya kuongezwa muda wa makubaliano hayo kutoka siku 5 hadi mwezi mmoja. Afisa huyo mwandamizi wa Yemen amesema hakuna matumaini kwamba Saudi Arabia itasitisha mapigano kwani tayari utawala wa Aal Saud umeshadidisha mashmambulizi dhidi ya miji kadhaa ya nchi hiyo siku mbili kabla ya kuanza kutekelezwa makubaliano hayo ya usitishaji vita. Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa kati ya jana na leo kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Saudia dhidi ya taifa la Yemen hususan katika mji wa Sa’ada.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa nchi zinazoendelea kupinga hujuma za Saudia dhidi ya Yemen huku Russia na China zikitaka vita hivyo visitishwe mara moja na njia za kisiasa kutumika kutatua mgogoro ulioko nchini Yemen. Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/…/48673-radiamali-ya-jeshi-la-yeme…