KIONGOZI WA MAPINDUZI YA KIISLAM AMESISITIZA KUTILIA UMUHIMU WA UZALISHAJI WA NDANI.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kutiliwa umuhimu uzalishaji wa ndani ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo ya nchi na kufanikisha uchumi wa kusimama kidete. Ayatullahil Udhma Khamenei amesema hayo Jumatano wakati aliponana na maelfu ya wafanyakazi wa kona zote za Iran na sambamba na kubainisha majukumu ya viongozi, taasisi na duru zote zinazoshughulikia masuala ya uzalishaji wa ndani akisema: Ufunguo wa kutatulia matatizo ya kiuchumi hauko Lausanne wala Geneva na wala New York, bali umo ndani ya nchi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza pia kuwa, watu wote nchini wanapaswa kulipa umuhimu mkubwa suala la uzalishaji wa ndani ya nchi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kutatua matatizo yaliyopo ya kiuchumi na kuongeza kuwa, vikwazo vya kidhulma vimekuwa na taathira katika kujitokeza matatizo hayo, lakini vikwazo hivyo haviwezi kuzuia jitihaza za umma na mipango mizuri iliyopangiliwa vyema, kwa ajili ya kustawisha uzalishaji wa ndani. Kiongozi Muadhamu vile vile ametolewa mfano namna taifa la Iran lilivyofanikiwa kupiga hatua kubwa za maendeleo ya kielimu na kitenolojia licha ya kwamba mashinikizo ya maadui wa taifa hili ni makubwa mno kwenye uwanja huo, na kusisitizia wajibu wa kutafutwa njia za ndani ya nchi kwa ajili ya kukabiliana na vikwazo vilivyopo vya kiuchumi.