Maadui wa Wilaya walitumia juhudi kubwa ili kubadilisha maana ya Wilaya, kwa kugeuza kituo cha Wilaya, wakati mwengine wanageuza asili halisi ya Wilaya, lakini yote haya yanategemewa kutoka kwa maadui. Jambo la kushangaza ni kwamba hata kama ulimwengu wote ukijitenga mbali na Wilaya, lakini vipi jumuiya ambayo ilikuwa inasikiliza Ghadir katika maisha yao yote ikae mbali na Wilaya. Hakika hili ni jambo chungu la kushangaza. Allah Azza wa Jallah ni shahidi juu ya ukweli huu kwamba milango ambayo Bibi Fatma (a.s) alipiga hodi mjini Madina bado hodi inapigwa hadi leo na yeye. Kuna watu mahususi ambao milango yao inapigwa hodi hata leo na Sayyida Fatma (a.s). Anawaambia kwamba mlifunga milango yenu na hamkutoa ushuhuda kwenye mfumo wa Wilaya wakati ule, lakini angalau basi katika zama zenu fungueni milango yenu na angalau katika zama zenu fungueni midomo yenu. Hii ndio hofu aliyokuwa nayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwamba Mola wangu kama Umma huu unachukuwa suala hili la msingi la Wilaya kwa wepesi basi matokeo yake yatakuwa nini? Allah Azza wa Jallah akasema kwamba Mjumbe wangu usiwe na hofu nao, niogope mimi na tangaza ujumbe wa Wilaya na uelezee kwa watu. Hata kama wale Maasumin kutoka katika kizazi chako ambao Allah Azza wa Jallah atawateua kama Mawali wake watabakia wakiwa wametengwa katika nyumba zao, watadhulumiwa, lakini bado wakati utakuja ambapo bendera ya Wilaya itanyanyuliwa tena. Na Ustadh Sayyid Jawwad Naqvi