Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari juu ya Kusherekea Kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), kwa hiyo siku ya kuzaliwa Imam Ali (a.s) tunaungana na dunia kuienzi amani, ambayo Imam Ali (a.s) ndio alieitilia Umuhimu.
Waislam, Wakristo,Masheikh, Wachungaji, Maskofu na Mapadri wanaamini kwamba utulivu wanaoupata katika sehemu zao za Ibada ni kwasababu ya kuenziwa Amani iliyopo.
Kiongozi yeyote wa kiroho awe Muslam au Mkristo atakapokuwa amani kwake sio muhimu huyo hatokuwa kiongozi wa Kidini.Tanzania iendelee kubakia kuwa kisiwa cha amani, maelewano kati ya Wakristo na Waslamu. Na: Twalha Zuberi Ndiholeye